Latest News
Loading...

Nchi kumi zilizotajwa kuwa sio salama kwa wanawake kutembelea wakiwa pekeyao…

Gazeti la Daily Mail ni moja ya Magazeti makubwa zaidi Uingereza na Ulaya, wataalamu wao wamefanya utafiti na kuyataja maeneo kumi ambayo siyo salama duniani kwa wanawake kutembelea kipindi cha mapumziko na sikukuu kama wakiwa peke yao.
  1. India: Jamaa wanasema huku kumekuwa na stori nyingi za matukio ya ubakaji wa wanawake, hii imefanya baadhi ya watalii kuwa na hofu ya kutembelea nchi hiyo. Ripoti hiyo inaonesha kunaripotiwa tukio la ubakaji kila ndani ya dakika ishirini.
  2. Brazil: Ripoti inaonesha matukio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia, wizi wa kutumia silaha ni tatizo kwa nchi hii. Matukio ya ubakaji yameongezeka kwa 157% kati ya mwaka 2009 na 2012.
  3. Uturuki: Huku nako ishu ni matukio ya ubakaji, yanashika kasi kila siku.
  4. Thailand: Ishu kubwa ni unyanyasaji wa kijinsia kwa upande wa huku, dawa za kulevya na pombe zimetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa.
  5. Egypt: Tokea kumetokea mapinduzi ya utawala 2011 hali haiku sawa bado, unyanyasaji wa kijinsia nako umeshika kasi kubwa.
  6. Colombia: Ripoti hiyo inaonesha Polisi wanadili kwa kiasi kidogo sana na ishu ya kulinda wanawake, ni mara chache watuhumiwa wa makosa ya ubakaji wamefikishwa Mahakamani.
  7. South Africa: Hii ni ya kwanza kutajwa kutoka Africa, unyanyasaji wa kijinsia, wizi wa kutumia silaha, na ubakaji ni matatizo makubwa sana kwenye nchi hii.
  8. Morocco: Watalii wa kike wanashauriwa kuvaa kama wenyeji wa nchi hii lakini ishu za ubakaji zinatajwa kwa kiwango cha juu kwa watalii wanawake ambao wanakuwa peke yao.
  9. Mexico: Japo Serikali imeweka nguvu nyingi kuhakikisha tu watalii wanakuwa salama, bado wizi wa kutumia silaha uko kwa hali ya juu sana pamoja na ubakaji wa wanawake kwenye vyombo vya usafiri wengi imewatia hofu.
  10. Kenya: Utalii imekuwa biashara kubwa kwa nchi hii, ripoti hiyo imeitaja kuwa unyanyasaji wa kijinsia uko kwa kiwango kikubwa sana kwa wanawake.