Mkazi wa Gongo la Mboto, Omary Hamis (25) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka tisa ambaye ni mlemavu wa kusikia na kuongea.
Hakimu Mkazi, Flora Haule wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, alisema mahakama imeridhishwa na ushahidi wa mashahidi tisa ukiwamo wa daktari na fomu namba tatu ya polisi (PF3), iliyotolewa mahakamani hapo kama kielelezo dhidi ya mshtakiwa huyo.
“Mahakama imekukuta na hatia hivyo inakuhukumu kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na kosa la kumlawiti mvulana wa miaka tisa ambaye ni mlemavu wa kusikia na kuzungumza, ili iwe fundisho kwa jamii,” alisema hakimu Haule.
Katika ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, ilidaiwa kuwa mtoto huyo siku ya tukio alifika kwenye banda la kuonyeshea video ambalo linamilikiwa na Hamisi saa za jioni, kwa ajili ya kuangalia video, lakini Hamis alimfukuza kutokana na kutokuwa na pesa ya kiingilio.
Baada ya kumfukuza mtoto huyo aliondoka, lakini baadaye alirudi bila ya Hamis kuwa na taarifa akakaa ndani ya banda na kisha kupitiwa na usingizi uliosababisha abaki kwenye banda hilo peke yake hadi usiku.
Hamis alitumia mwanya huo kumlawiti mtoto huyo kwenye jumba bovu lililopo jirani na ofisi yake hiyo.
Mashahidi waliieleza mahakama kuwa walisikia sauti ya mtu ambayo ilikuwa haisikiki vizuri akiomba msaada, ndipo waliposogea na kumkuta Hamis akitekeleza kitendi hicho huku akijua kuwa ni kosa kisheria.
Mashahidi walidai hata walipomkaribia, Hamis aliendelea kutekeleza kitendo hicho hadi walipolazimika kumpiga mateke. Hamis alikiri kuwa siku hiyo watoto walifika kwenye banda lake hilo.
Wakili wa Serikali, Ester Kyara aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wote wanaotumia mabanda ya kuonyesha video kufanya ukatili kwa watoto.
Katika utetezi wake, Hamisi alisema ana familia inayomtegemea hivyo apunguziwe adhabu, maombi ambayo yalitupiliwa mbali na mahakama hiyo na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Hamisi anadaiwa kutenda kosa hilo Agost 26, 2014 eneo la Gongo la Mboto.
Latest News
Loading...
Afungwa Kifungo cha Maisha Jela Kwa Kumlawiti Mtoto Mlemavu wa kusikia na kuongea.
Related Posts:
Jeshi la Tanzania JWTZ Walioko Kongo Watajwa Kuwa Kati ya Majeshi 35 Bora Duniani.... HONGERA JWTZ KWA KUTOA KIKOSI BORA NA MADHUBUTI CHA KIJESHI DUNIANIMajarida mbalimbali duniani yamechapisha makala juu ya vikosi 35 bora zaidi vya jeshi duniani huku kikosi cha JWTZ Monusco kilichoko Jamhuri ya Kidemokrasia… Read More
Juma Duni Haji Aikosoa CHADEMA Juu ya Muundo Wake Aliyekuwa mgombea Mwenza wa Rais kwa tiketi ya Chadema, Juma Haji Duni ambaye wiki hii amerejea katika chama chake cha awali cha CUF amekosoa muundo wa uongozi wa chama hicho alichojiunga nacho mwaka jana ili kutimiza matak… Read More
Aunt Ezekiel Atumbuliwa Jipu Na Serikali Ya Magufuli, Ipo Hapa Kaulimbiu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ‘JPM’ ya kutumbua majipu na watu wasiolipa kodi imemdondokea staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson baada ya gari lake aina ya Audi kukamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanza… Read More
Jerry Muro Afunguka Haya Kuhusu Rais John Pombe Magufuli Baada ya Kumfuta Kazi Anne Kilango Msemaji wa Timu ya Yanga amefunguka kuhusu Rais Magufuli mara tu baada ya kutengua Ukuu wa Mkoa wa Anne Kilango huko Shinyanga....Ameandika haya katika mtandao wake:"Huyu ndie Rais ambae Mungu amemsisha katika taifa la Tan… Read More
Clouds FM Yaendeleza Nyakua Nyakua ya Watangazaji na Madj..Wamewachukua Hawa East Africa Radio Ile Vuta N’kuvute ya vituo vya redio inaendelea na sasa East Africa Radio imekuwa mhanga mpya.Dj wa kike, Sinyorita na mtangazaji wa The Cruise, Mami wanadaiwa kuondoka East Africa Radio kuanzia wiki hii baada ya kupata dau… Read More
0 comments:
Post a Comment