Kaulimbiu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ‘JPM’ ya kutumbua majipu na watu wasiolipa kodi imemdondokea staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson baada ya gari lake aina ya Audi kukamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa tuhuma za kuingizwa nchini kinyemela bila kulipiwa ushuru na kukwepa kodi.
Habari kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zilieleza kuwa tukio la Aunt kutumbuliwa lilijiri hivi karibuni ambapo staa huyo alikuwa akificha siri hiyo isinaswe na mapaparazi wetu, jambo ambalo limemshinda.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilimsaka Aunt kutaka kujua kisa kamili ambapo alipobanwa alikiri kukamatwa kwa gari lake hilo kwa makosa ya kukwepa kodi wakati linaingizwa Bongo hivyo kuwa mikononi mwa TRA.
“Kweli gari langu limeshikiliwa na TRA ila haina tatizo sana kwani wamekagua, karibia kila kitu kipo sawa isipokuwa ninadaiwa kodi tu ambayo nayo si fedha nyingi kiasi cha kunishinda. Waliniambia vibali vyake vyote viko sawa na kwamba lipo nchini kihalali kabisa hivyo ninachotakiwa kulipia ni kodi tu ambayo najipanga kulipia muda wowote.
“Nilishtuka sana baada ya kukamatwa kwani nilihisi ndiyo mwisho wa kuwa na gari langu lakini sasa nimepata moyo baada ya kuambiwa hakuna kilichochakachuliwa.
“Natafuta Sh. milioni 10 na kitu ili niweze kulikomboa,” alisema Aunt aliyedai gari hilo alinunuliwa na baba mtoto wake, Moses Iyobo ‘Moze’ huku akigoma kutaja bei yake.
-GPL
Latest News
Loading...
Aunt Ezekiel Atumbuliwa Jipu Na Serikali Ya Magufuli, Ipo Hapa
Related Posts:
Picha: Ndege ya kwanza ya ATCL yatua Dar Hatimaye mwali amewasili. Ni ndege ya kwanza ya ATCL, Bombadier Q400 NextGen. Bombadier Q400 NextGen baada ya kuwasilia JNIA, Dar Jumanne hii Ndege hiyo imetokea Canada ilikotengenezwa na kupokelewa kwa shangwe huku mapoke… Read More
PICHA: Hizi ndio Kampuni 10 za Ndege zenye usalama zaidi duniani Mtu wangu naamini utakua unakumbuka jinsi ajali za ndege zilivyochukua headlines miaka michache iliyopita, hali hiyo imefanya makampuni ya usafirishaji wa ndege duniani kuboresha huduma zao kwa kununua ndege za gharama … Read More
Kampuni ya Benchmark Productions ya Madam Rita yafungiwa, inadaiwa Tsh Bilioni 7 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kushirikiana na Kampuni ya Udalali ya Yono, wameifungia Kampuni ya Benchmark Productions na kuipa muda wa siku 14, iwe imelipa deni la kodi ya Sh bilioni 7.04, vinginevyo mali za k… Read More
MSAJILI WA VYAMA ASEMA : Sikumrudishia Lipumba uenyekiti CUF, Kajirudisha Mwenyewe Kinyemela Wakati wanasiasa na wasomi wakimnyooshea kidole Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (pichani) kwa uamuzi wake wa kumtambua aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, mwenyewe ameibuka na k… Read More
AUDIO: Taarifa ya Polisi kuhusu ajali ya Basi la New Force Njombe Septemba 19 majira ya saa moja na nusu katika kijiji cha Lilombwi kata ya kifanya Barabara ya kuu ya Njombe – Songea kulitokea ajali iliyohusisha basi la New Force lenye namba za usajili T 429D… Read More
0 comments:
Post a Comment