Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kwa makamu mwenyekiti wake Jerome Msemwa, April 3 imetoa tamko kuhusu zile tuhuma za upangaji wa matokeo kwa mechi za Ligi daraja la kwanza zilizokuwa zinazihusisha timu za kundi C.
Timu za Geita Gold ya Geita, JKT Oljoro ya Arusha na Polisi Taboraya Tabora zimekutwa na hatia ya kosa la upangaji matokeo na hivyo zote zimeshushwa Ligi daraja la pili na JKT Kanembwa imeshushwa hadi Ligi ya mkoa sababu tayari ilikuwa imeshuka kutoka Ligi daraja la kwanza..
Kamati ya nidhamu pia imewafungia refa Saleh Mang’ola na kamisaa wa mechi ya JKT Kanembwa dhidi ya Geita Gold Moshi Juma kutojihusisha na soka maisha, na kamati pia itatangaza baada ya kupitia kanuni ni timu ipi imepanda Ligi kuu na ipi imepanda daraja la kwanza.
Hii ni List ya watu wote waliokumbana na adhabu ya kamati ya nidhamu
- Kocha msaidizi wa Geita Gold Choke Abeid amefungiwa maisha kutojihusisha na soka.
- Magolikipa Mohamed Mohamed wa JKT Kanembwa na Dennis Richard wa Geita Gold wamefungiwa miaka 10 na faini milioni 10 kutojihusisha na soka.
- Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Yusuph Kitumbo, Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Fateh Remtullah, Mwenyekiti wa klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita na kocha msaidizi wa Polisi Tabora, Bernad Fabian wamefungiwa maisha kutojihusisha na mpira wa miguu.
- Mwamuzi wa mchezo kati ya Polisi Tabora v JKT Oljoro, Masoud Mkelemi na mwamuzi wa akiba, Fedian Machunde wamefungiwa kwa muda wa miaka kumi kutojihusisha na mpira wa miguu, na kutozwa faini ya shilingi milioni (10,000,000) kumi kila mmoja.
Latest News
Loading...
Kimenuka tena TFF, Watu wamefungiwa soka maisha leo!!
Related Posts:
ORIGI AMEANZA KUELEWEKA LIVERPOOL Divock Origi ametupia kambani bao mbili akitokea benchi kwenye mchezo wa Premier League ambao Liverpool imepata ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Stoke na kupanda kwa nafasi moja hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi. S… Read More
Matokeo ya Mechi ya Yanga na Kagera Sugar Iliyochezwa leo Jioni Haya Hapa Michezo ya viporo ya Ligi Kuu soka Tanzania bara imepigwa leo kwa vilabu vya Azam FC na Yanga kucheza michezo yao ambayo awali ilikuwa imehairishwa kutokana na kuingiliana na michezo yao ya Kombe la Shirikisho barani Afrik… Read More
Mgao wa Fedha za Mbwana Samatta Kuuzwa Genk Zaanza Kuleta Zengwe Klabu ya Simba... TP Mazembe imemuuza Mbwana Samatta kwa KRC Genk ya Ubelgiji ikadaka fedha zake, jambo la kushangaza hadi leo Simba haijalipwa sehemu ya fedha hizo kwa mujibu wa mkataba.Simba ilipomuuza Samatta kwa TP Mazembe ya DR Congo, m… Read More
STEWART HALL AFICHUA SIRI YA USHINDI AZAM VS EPERANCE KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, amesema mabadiliko aliyofanya kipindi cha pili kwa kiasi kikubwa yamechangia ushindi wa mabao 2-1 walioupata dhidi ya Esperance ya Tunisia. Mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ko… Read More
PAZIA LA SPORTS XTRA NDONDO CUP 2016 KUFUNGULIA LEO Dr. Juma Mwaka (kushoto) akimkabidhi kombe la Ndondo Cup nahodha wa Faru Jeuri Selemani Bujji baada ya timu yake kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka 2015 Pazia la msimu mpya wa Sports Extra Ndondo Cup 2016 linafunguliwa l… Read More
0 comments:
Post a Comment