Bunge limesimamisha utekelezaji wa miradi yote mipya ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mpaka hapo Kamati na Wizara itakapopitia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), sambamba na kuitisha taarifa za utekelezaji wa miradi yote iliyofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.
Aidha, imeagiza ukaguzi wa kina wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Makamu wa Rais kwa kuangalia usalama wa jengo, hesabu zilizotumika kama zinaendana na thamani ya jengo na kama washauri walitoa ushauri wao ipasavyo.
Akizungumza katika kuhitimisha ukaguzi wa miradi mbalimbali ya serikali iliyofanywa na Kamati ya Katiba na Sheria, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa alisema NSSF ilitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ikiwa haijitoshelezi kwa kutoonesha gharama zilizotumika mpaka sasa, bajeti iliyopangwa kutumiwa na kiasi kilichosalia ili kubaini kama fedha zilizotumika zinalingana na thamani ya ujenzi wenyewe.
Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa takribani siku tano kuanzia Machi 29, mwaka huu, ilitembelea Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu na Mahakama.
Akizungumzia taarifa za utekelezaji wa miradi iliyofanywa na mifuko yote ya hifadhi za jamii, Mchegerwa alisema kamati yake inataka kupitia taarifa zote za utekelezaji wa miradi sambamba na kupitia sera ya uwekezaji ili kuangalia kama yamefuata taratibu na hakuna upotoshaji.
“Kwanza kuna madeni makubwa ambayo mifuko hiyo inadai kwa wapangaji wao. Pia tunaangalia sera ya uwekezaji ili kujiridhisha kama ushauri wa kitaalamu uliotolewa unakidhi matakwa ya ujenzi unaoendelea.
Aliongeza: “Kuna majengo mengi yamejengwa hayana wapangaji lakini sera ya uwekezaji itatusaidia kujua kama inafuatwa. Pia itatusaidia kubaini mapungufu yaliyojiri, maana wajumbe wengi wana wasiwasi kuwa huenda ujenzi wa majengo unalenga kwa wahusika kupata asilimia 10 bila kuangalia mahitaji halisi, kwani majengo mengi yako wazi.”
Latest News
Loading...
NSSF Yapigwa Marufuku Ujenzi wa Miradi Mipya
Related Posts:
Mwanamuziki Tunda Man Apata Ajali Mbaya ya Gari Akiwa na Wenzake Watano..Taarifa za Kifo na Majerui ipo Hapa Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakua umekutana na taarifa inayomhusisha Tunda Man kupata ajali akiwa Mkoani iringa Asubuhi ya April 17 millardayo.com imempata Tunda Man mwenyewe na amekubali kutuelezea.Mael… Read More
DARAJA la Kigamboni Laanza Kutumika Kwa Mbwembwe...Wengine Wafanya Kama Sehemu ya Kivutio Baada ya Serikali kuruhusu matumizi ya daraja jipya la Kigamboni kwa watembea kwa miguu na magari kwa majaribio, hatua hiyo imepeleka neema kwa wakazi wa mji huo, huku ikipunguza idadi ya vyombo vya moto katika vivuko. … Read More
Mhasibu Wa Halmashauri Ya Singida Afikishwa Mahakamani Akituhumiwa Kupokea Milioni 29 za Watumishi HEWA MHASIBU wa Halmashauri ya wilaya ya Singida, Imani Abduli Nyamangaro (44) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida akikabiliwa na tuhuma za mashitaka 57 ya wizi wa mishahara hewa yenye jumla ya shilin… Read More
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi William Lukuvi Aziponda Nyumba Zinazojengwa na NHC,PPF WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema hakuna taasisi ya Serikali wala binafsi nchini iliyojenga nyumba za bei nafuu. Kutokana na hali hiyo, amesema Serikali imekusudia kuanzisha Sheria ya… Read More
Rais Magufuli Awataka Mawaziri wasioweza Kazi Bila Posho au Safari Wajiondoe Wenyewe Viongozi serikalini wakiwemo mawaziri na makatibu wakuu, wameombwa na Rais John Magufuli, kuvumilia machungu wakati wa uongozi wake, kama ambavyo wananchi walivyovumilia tangu Uhuru. Amesema hayo jana wak… Read More
0 comments:
Post a Comment