Ofisi ya Elimu wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani imelazimika kuwapa likizo walimu saba wa Shule ya Msingi Mingwata ili kuwajenga kisaikolojia baada ya kukithiri kwa matukio ya kishirikina yanayowakumba katika shule hiyo.
Walimu hao wanakumbana na matukio ya ajabu ikiwamo kujikuta uchi, kupigwa fimbo na mtu asiyeonekana na kulazwa nje ya nyumba zao.
Mmoja wa walimu walioathirika na matukio hayo, Emmanuel Shaaban alisema yeye na familia yake hawana raha kutokana na matukio hayo kwa kuwa usiku huvuliwa nguo na kujikuta wamelazwa sehemu nyingine, huku wakiwa wamechanjwa kwa wembe mwili mzima.
“Tarehe 26 mwezi wa pili, siku ya Alhamisi sitaisahau kabisa. Ndiyo siku ambayo nilikatwa viwembe mwili mzima na hali yangu ilikuwa mbaya, niliishiwa nguvu na mwili ukawa na ganzi na nilipokwenda hospitali niliambiwa sina ugonjwa,” alisema Shaaban.
Alisema alipotoka hospitali alikwenda kijijini kwao mkoani Mwanza na huko aliendelea kuwa na hali mbaya kutokana na kuzimia mara kwa mara kwa sababu ya maumivu ya kichwa hadi alipotibiwa kienyeji.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mikidadi Mbelwa alisema awali alikuwa akiona vituko usiku na mchana, lakini alivumilia huku akitunza siri bila kuwaeleza wenzake ili asiwakatishe tamaa.
Mbelwa alisema baadhi ya matukio aliyokutana nayo ni kuvuliwa nguo usiku, kulazwa eneo jingine, kuchapwa viboko, kumwagiwa damu kwenye korido ya nyumba, kuchanjwa kwa wembe, kuzungukwa na nyoka mwilini, kuona mtu na kisha anapotea na kutupwa kwenye mashimo.
Mzazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo, Asha Kondo alikiri kuwapo kwa matukio ya watoto kuugua na kuanguka hadi uongozi wa kijiji ulipopeleka mganga wa kienyeji kutoa kinachodaiwa ni uchawi.
Mratibu wa Elimu wa Kata ya Marui, Damaru Charles alisema amekuwa akipokea malalamiko hayo na kuyawasilisha ngazi za juu.
Ofisa Elimu Msingi wilayani hapa, Aurelia Rwenza alisema tatizo hilo linawapa shida walimu na kurudisha nyuma maendeleo ya elimu katika sehemu hiyo.
“Kwa kweli walimu wameathirika, hivi sasa tunatakiwa kuwajenga kisaikolojia,” alisema.
Latest News
Loading...
Walimu Walazwa UCHI na Kuchapwa Viboko
Related Posts:
Mwisho Mwampamba Kortini..Alala Mahabusu Siku Mbili Kisa Matusi ya Nguoni... MOROGORO: Ikiwa takriban siku 40 tangu baba yao, Dk. Ephraim Njawala Mwampamba, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) afariki dunia, mwanaye Mwisho Ephraim Mwampamba ameburuzwa mahakamani na kaka yake, Robert… Read More
Serikali yadhamiria kurejesha heshima ya wazee nchini SERIKALI imesema imedhamiria kurejesha heshima ya wazee wote hapa nchini kwa kuisimamia jamii kuwathamini wazee na kuwapa kipaumbele katika huduma zote za jamii. Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Afya Maendeleo ya… Read More
Taarifa Kwa Umma: Kufutwa Kwa Safari za Ndege za Fastjet April 02, 2016 TAARIFA KWA UMMA;KUFUTWA KWA SAFARI ZA NDEGE APRILI 2, 2016Tunaomba radhi sana kwa taarifa kwamba idadi kadhaa ya abiria wetu walishindwa kufika kwenye maeneo waliyokusudia jioni ya Aprili 2, 2016.Hii ilitokana na kushindwa … Read More
Hivi Ndivyo Irene Uwoya Alivyojifungua Kwa Upasuaji Bila Ganzi Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema hakupenda kabisa kujifungua kwa upasuaji lakini ilimbidi afanye hivyo ili kuokoa maisha yake pamoja naya mwanaye.Muigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Krish, amekiambia kip… Read More
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda Apiga Marufuku kilevi aina ya Kiroba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa huo. Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati … Read More
0 comments:
Post a Comment