Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyopo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Mheshimiwa Odinga ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga, wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02 April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe Mama Janeth Magufuli.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao, kwa lengo la kumsalimia.
"Nimekuja kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike, na vilevile kuja kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa Chato, na nilisema siendi Dar es salaam nitakuja hapahapa Chato" Alisema Mheshimiwa Odinga.
Pamoja na kukutana na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pia amemsalimu Mama wa Rais Bibi Suzana Joseph Magufuli na pia amezulu Makaburi walimozikwa wanafamilia wa Rais, akiwemo Baba Mzazi Mzee Joseph Magufuli.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga nyumbani kwake Chato mkoani Geita mara baada ya Kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana na Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuwasili Chato.
Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwa na Rais John Magufuli, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Raila Odinga Bi. Ida Odinga wakisali kwenye makaburi ya familia ya Mhe. Rais Chato Mkoani Geita.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na mama mzazi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bi Suzana Joseph Magufuli mara baada ya kuwasili Chato Mkoani Geita.
Latest News
Loading...
Home »
KITAIFA
» Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya RAILA ODINGA amtembelea Rais Dkt JOHN MAGUFULI Nyumbani Kwake CHATO
Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya RAILA ODINGA amtembelea Rais Dkt JOHN MAGUFULI Nyumbani Kwake CHATO
Related Posts:
Mbunge wa Zamani na Moshi Vijijini (CCM) Apandishwa Kizimbani Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Thomas Ngawaiya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la kujenga hoteli kwa kutumia makandarasi wasiosajiliwa. Ngawaiya ambaye aliwahi… Read More
Hamad Rashid: Serikali ya Muungano isibabaishwe na wahisani Mjumbe wa Kuteuliwa wa Baraza la Wawakilishi, Hamad Rashid (ADC) ametaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutobabaishwa na nchi washirika wa maendeleo kwa kususa misaada yao kwa kile alichosema, nafasi ipo … Read More
Watu Watano Wafariki Dunia Jijini Dar Kwa Kuangukiwa Na Kifusi. Watu watano wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa, baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuangukiwa na kifusi na mti wakiwa wamelala, ajali hiyo ilisababishwa na kupasuka kwa karo la majitaka la nyumba ya jirani… Read More
Viongozi CUF washutumiwa kwa kukosa uzalendo Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekishiutumu Chama cha Wananchi (Cuf) pamoja na viongozi wao kwa kukosa uzalendo kutokana na kauli zao za kuunga mkono wahisani kuisitishia misaada Tanzania. Hayo yalise… Read More
Bajeti ya Serikali 2016/ 2017 ni Trilioni 29.5.....Matumizi ya Kawaida ni Trilioni 17.7, Mikopo ni Trilioni 11.1. Bofya Hapa Kuona Vipaumbele Vilivyotajwa Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano itaizidi ya Serikali ya Awamu ya Nne kwa Sh7.1 trilioni baada ya Waziri wa Fedha kutangaza sura ya bajeti ya mwaka 2016/17 inayoonyesha kutakuwa na makusanyo na matumizi ya … Read More
0 comments:
Post a Comment