Septemba 19 majira ya saa moja na nusu katika kijiji cha Lilombwi kata ya kifanya Barabara ya kuu ya Njombe – Songea kulitokea ajali iliyohusisha basi la New Force lenye namba za usajili T 429DEU.
millardayo.com na Ayo TV imempata Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Prudensiana Protasi, ameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendokasi wa basi hilo uliosababisha basi hilo kumshinda Dereva ambaye hata hivyo alikimbia baada ya tukio kutokea.
Aidha taarifa kutoka kwa Kamanda huyo zinasema ajali imesababisha vifo vya watu 12 na majeruhi 28 ambapo majeruhi 16 walitibiwa na kuruhusiwa. Majeruhi 9 kati ya waliofikishwa katia Hospitali ya mkoa wa Njombe, Kibena hali zao zinaendelea vizuri huku wanne wakiwa kwenye hali mbaya na kupelekwa mkoani Ruvuma kwa matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment