Mfanyabiashara na bilionea w 21 Afrika Mohammed Dewji ameanza kutekeleza baadhi ya ahadi zake ndani ya klabu ya Simba, Dewji ambaye ameomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kwa Tsh bilioni 20, ameanza kutekelez ahadi zake ambazo alisema atafanya hivyo wakati Simba inaelekea katika mfumo wa mabadiliko ya kiuendeshaji.
Dewji ambaye anasubiri mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji kutoka katika mfumo wa sasa na kuiingiza klabu ya Simba katika mfumo hisa, ameanza kulipa mishahara ya wachezaji wa Simba na sekretarieti ambayo kwa sasa timu hiyo haina udhamini, kupitia kwa taarifa ya Simba ambayo imetangaza kumshukuru MO.
Imeeleza MO kuanza kulipa mishahara ya wachezaji na amekubali kulipia kodi nyasi bandia zitakazoletwa nchini kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa Simba, lakini pamoja na hayo taarifa ya Simba inaeleza MO ataendelea kusaidia klabu hiyo gharama za uendeshaji hadi kipindi cha mpito cha miezi sita kitakapomalizika
.
.
0 comments:
Post a Comment