Michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya katika msimu huu wa mwaka 2016/17 imeendelea usiku wa wa tarehe 27/9/2016 kwa takribani makundi manne kuingia dimbani Leicester city wakicheza katika dimba lao la king power wamepata ushindi wa pili katika michuano ya ulaya kwa kuichapa FC Porto kwa bao 1-0.
Real madrid wakicheza ugenini katika uwanja wa Signal iduna Park wametosha nguvu na wenyeji Borrusia Dortmund kwa kufungana mabao 2-2. Nao Monaco wakiwa nyumbani wakatoka sare ya 1-1 na Bayer Leverkusen.
Wareno wa Sporting Lisbon wamewafunga timu ya Legia Warszawa toka Poland kwa mabao 2-0 FC Copenhagen wameibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Club Brugge
Juventus wameibuka na ushindi ugenini kwa kuichapa Dinamo Zagreb mabao 4-0,Sevilla wameshinda 1-0 dhidi ya Lyon huku Tottenham ikichomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji CSKA Moscow.
0 comments:
Post a Comment