Latest News
Loading...

Ripoti: Angelina Jolie aomba talaka kwa Brad Pitt

Na hawa pia? Ni swali ambalo unaweza kujiuliza uliposoma tu kichwa cha habari. Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, Angelina Jolie ameomba talaka kwa mume wake, Brad Pitt.
angelina-jolie-brad-pitt_0
Wawili hao walifunga ndoa miaka miwili iliyopita, lakini wamekuwa pamoja kwa zaidi ya muongo sasa. Wamekuwa pamoja tangu mwaka 2004 na wana watoto sita, Maddox, Pax, Zahara, Shiloh, Vivienne, na Knox.
rs_1024x696-151016085525-1024-2-angelina-jolie-family-vogue-jl-101515
Nyaraka za kuomba talaka hiyo zimewasilishwa September 15. Jolie anataka aishi na watoto wote huku akiomba Pitt apewe ruhusa ya kuwasilimia.
TMZ imedai kuwa Jolie alikuwa hakubaliani na jinsi Pitt anavyowalea watoto wake. Jolie na Pitt walikutana mara ya kwanza kwenye filamu ya mwaka 2003, Mr. & Mrs. Smith.

0 comments:

Post a Comment