Latest News
Loading...

Utafiti: Watanzania milioni 5.4 hawajui kusoma na kuandika

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na mashirika ya kimataifa, umeonesha kuwa Watanzania milioni 5.4 hawajui kusoma na kuandika.
kaimu-katibu-mkuu-dk-leonard-akwilapo
Akizungumza katika shirika la elimu duniani UNESCO, naibu katibu mkuu sayansi, elimu na teknolojia, Dk Leonard Akwilapo, amesema takwimu hizo za kuongezeka watu wasiojua kusoma zinahitaji juhudi za serikali ili kufikia malengo ya kimataifa.
“Kuna takwimu imetolewa ambayo siyo nzuri sana, kwamba Tanzania tuna takribani watu milioni 5.4 ambao hawajui kusoma na kuandika, sasa hilo ni janga kubwa sisi tunaliona, na tunatengeneza landmark kuhakikisha kwamba tunaondoa tatizo kama hili, kuhakikisha ili watu wote wawe na elimu, sisi tunaamini mtu akishakuwa na elimu ya msingi basi anaweza akajiendeleza katika fani zingine na sekta zingine,” alisema Akwilapo.
BY: EMMY MWAIPOPO

0 comments:

Post a Comment