Septemba 24 2016 klabu ya Man United ya England ilicheza mchezo wake wa sita wa Ligi Kuu England huku ikiwa na kumbukumbu ya vipigo vitatu mfululizo, Man United safari hii ilishuka katika dimba lake la Old Trafford kuikaribisha Leicester City ambao ni Mabingwa watetezi wa EPL.
Tofauti na wengi walivyotegemea kuwa huenda Man United wakapokea kipigo cha nne kutokana na kucheza na Bingwa mtetezi Leicester City ambaye msimu uliopita aliwatoa jasho timu vigogo wa EPL, leo wamefanikiwa kubuka na ushindi wa goli 4-1, kingine kilichovutia ni mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba alifunga goli lake la kwanza.
Katika ushindi huo wa goli nne za Man United zilifungwa na Chris Smalling dakika ya 22, Juan Mata dakika ya 37, Marcus Rashford dakika ya 40 na Paul Pogba ambaye alikuwa akibezwa kutokana na kutofunga akafunga goli la nne dakika ya 42 na kuwaacha Leicester wakiishia goli moja lililofungwa na Demarai Gray dakika ya 60.
0 comments:
Post a Comment