Timu ya Singida United imerejea kwenye ligi msimu huu baada ya kusota bondeni kwa muda mrefu, lakini wamerejea kwa kishindo kwa kuwa ni miongoni mwa vilabu ambavyo mfuko wao wa salio umetuna kutokana na pesa za wadhamini.
Singida wana wadhamini rasmi watatu (YARA, SportPesa na Puma) wana wadau pia wanaowawezesha kama NMB Bank, DTB Bank na Oryx wote hao wanaingiza mtonyo ndabi ya Singinda United huku klabu hiyo ikitarajia kutangaza wadhamini wengine wawili hivi karibuni.
Mkurugezi wa Singida United Festo Sanga ametaja wadhamini na wadau wote wa klabu yao na kiasi cha pesa wanachowapa kwa mwaka.
“Tuna udhamini mkubwa kutoka YARA ambao wanatoa zaidi ya shilingi milioni 300 za Tanzania kwa mwaka mmoja, tuliwafuata na walikuwa mwisho kwenye budget yao kwa hiyo wametuahidi kwenye budget ijayo mambo yatakuwa mazuri zaidi,” Festo Sanga.
“Mmdhamini wetu mwingine ni SportPesa ambaye anatoa zaidi ya shilingi milioni 250 kwa mwaka. Udhamini mwingine tumepata kutoka Puma wa zaidi ya shilingi milioni 120.”
“Oryx ni wadau wetu (sio wadhamini) wametupa zaidi ya shingi milioni 100, hawataki kujionesha kama wanatudhamini kwa sababu program yao kubwa ya kuidhamini Singida United itaanza mwaka ujao. DTB Bank ni wadu wetu wengine waliotupa zaidi ya shilingi milioni 20, NMB wametupa milioni 10 kwa ajili ya kui-support klabu.”
Ukifanya hesabu ndogo hapo utagundua Singida United wanatengeneza zaidi ya shingi milioni 800 kwa mwaka kutoka kwa wadhamini na wadau wao sawa na kiasi inachopata klabu ya Simba kutoka kwa wadhamini wao SportPesa kwa mwaka wa kwanza wa udhamini huo
NMB na DTB ni kambuni mbili zenye ushindani wa kibiashara lakini wote wanaiunga mkono Singida United, hawa sio wadhamini ni wadau tu hawana mkataba wa udhamini na klabu hiyo.