Latest News
Loading...

“Natarajia kuwa na timu bora mara mbili ya Serengeti Boys iliyopita”-Kocha Milambo


Na Thomas Ng’itu
Kocha Oscar Milambo wa Serengeti Boys ametamba kutengeneza kikosi kipya cha Serengeti Boys na kuwa imara zaidi ya kikosi cha mara ya kwanza.
Milambo akipiga stori na ShafihDauda.co.tz alifunguka wameanza maandalizi ya mapema ili kupata kikosi imara kwaajili ya michuano ya chini ya miaka 17 inayotarajiwa kufanyika 2019 nchini Tanzania.
“Tulianza mapema kutafuta vijana muda mrefu,tulifanikiwa katika hilo kwasababu tumewaweka kambini baada ya michujo ya awali,lakini bado tunaendelea na mchujo zaidi kwasababu tunataka kufanya mambo makubwa zaidi,” Milambo.
Akizungumzia changamoto aliyokutana nayo, wachezaji wake kuchelewa kujiunga na kambi kutokana na kuwa katika mitihani, imewafanya kushindwa kwenda na kasi ya wenzao lakini hata hivyo amesisitiza kuliweka sawa jambo hilo.
“Wachezaji baadhi walikuwa wapo katika mitihani ya la saba,wasingeweza kuacha kufanya na tayari wameanza kuwasili na wengine leo wameanza mazoezi,bado hawajawa fiti kwasababu wenzao waliwatangulia lakini watakua poa.”
Milambo aliomba watanzania wawe nae bega kwa bega katika kuendeleza soka la vijana, huku akisisitiza kuwa anaamini watafanya vizuri katika michuano hii kutokana na kutokuwa na ugeni kama ilivyokuwa kwa mara yao ya kwanza kushiriki.


0 comments:

Post a Comment