Obama akimshika begani Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya
Mandela nchini Afrika Kusini. Kulia ni Michelle Obama akiwa amenuna.
RAIS wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle wanadaiwa kutengana. Habari zinadai kuwa wawili hao wanalala katika vyumba tofauti kwa sasa ndani ya Ikulu ya Marekani 'White House'.
Mgogoro baina ya wawili hao ulianza zamani na wameweza kuendelea kuishi pamoja kwa sababu ya watoto wao wawili wa kike Sasha na Malia na kulinda heshima ya urais.
Michelle anadai amechoka na atakutana na mwanasheria wa masuala ya talaka ili aweze kuachana na rais huyo wa 44 nchini Marekani. Michelle ataendela kuishi Ikulu 'White House' kwa muda wote uliobaki katika kipindi cha utawala wa Obama, ila ameweka wazi kuwa watakuwa wakiishi vyumba tofauti.
Anataka kuishi katika chumba kimojawapo cha familia kilichowazi na anajiandaa kuhamisha nguo zake na kila kilicho chake kutoka kwenye jumba lao la kifahari la mamilioni ya dola lililopo Chicago.
Michelle alichanganyikiwa zaidi baada ya Obama kupiga picha za kimahaba akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya marehemu Nelson Mandela nchini Afrika Kusini.
Obama mwenye miaka 52, alikuwa akifurahi, kunong'enezana na kumshika begani mrembo huyo mwenye umri wa miaka 46 ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Denmark tangu Oktoba 3, 2011.
CHANZO: nation.com