Latest News
Loading...

Majina ya watu 4 matajiri zaidi Tanzania

Uchumi mkubwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unategemea zaidi kilimo kwa takriban asilimia 25 ya pato la taifa na asilimia 85 bidhaa zinazouzwa nje ya nchi. Aidha, Tanzania ina madini kama dhahabu, almasi, makaa ya mawe, uraniamu, chuma, shaba, Tanzanite na mengine lukuki.
Toka kuaga sera za kijamaa katikati mwa miaka ya 1980, ambako pia Mwalimu Nyerere aling’atuka kupisha utekelezaji wa sera za kibepari, Tanzania imetengeneza matajiri wengi. Katika makala hii fupi, tumekusanya majina ya Watanzania wanne, ambao ndio matajiri wakubwa zaidi nchini Tanzania, kwa mujibu wa jarida maarufu duniani la Forbes.
4) Reginald Mengi – Thamani: $560 Million
Bwana Reginald Mengi ni mmiliki wa moja ya kampuni kubwa inayomiliki vyombo vya habari ya IPP  Media Group, yenye magazeti 11, stesheni za redio na TV na mitandao ya intaneti.
3) Said Salim Bakhresa – Thamani: $575 Million
Umri wake ni miaka 65, na yeye alianza mwenyewe mpaka kufikia hapo. Mfanyabiashara huyu ameanzisha Azam TV, yenye mfumo wa kulipia chaneli za TV Afrika ya Mashariki. Aliacha shule akiwa na miaka 14 na kuanza kuunza Mix (Urojo) na baadae kufungua mgahawa mdogo eneo la Livingstone Kariakoo jijini Dar Es Salaam, na kisha kuhamia katika biashara ya mazao ya kilimo. Katika miongo minne iliyopita  ameongeza mauzo yake kwa dola za kimarekani milioni 750, na kuifanya Bakhresa Group kuwa moja ya kampuni kubwa Afrika ya Mashariki kwa kuwa na wafanyakazi zaidi ya 5,000 na kujikita zaidi kwenye bidhaa za vinywaji na chakula, Upakiaji wa bidhaa, huduma za feri na Mafuta ya Petroli na usafirishaji.
2) Rostam Aziz –Thamani: $1 Billion
Mnamo mwezi Mei mwaka 2014 aliuza hisa zake 17% alizokuwa akimiliki katika kampuni ya Vodacom. Vile vile ana miliki kampuni Caspian Mining, inayojihusisha na uchimbani wa madini kwenye kampuni kubwa kama BHP Billiton na Barrick Gold. Kampuni hiyo ya Caspian Mining pia inamiliki sehemu kubwa ya ardhi yenye uwezekano wa kuwa na madini kama dhahabu, chuma na shaba hapa Tanzania. Aidha, Rostam ana hisa katika Bandari ya Dar es salaam ambapo yuko pamoja na Hutchison Whampoa na ana miliki sehemu ya ardhi kubwa hapa Tanzania, Dubai, Oman na Lebanon.
1) Mohammed Dewji – Net Worth: $1.3 Billion
Ana umri wa miaka 40, na ndio mdogo kuliko matajiri 50 wa Afrika yote kwa mfululizo wa miaka 3 sasa, ana miliki 75% ya kampuni ya METL Group, inayohusika na viwanda nchini humu iliyoanzishwa na Baba yake. Kizuri kuhusu Mohammed Dewji aliibadisha nyumba ya kufanyia manunuzi ya bidhaa za kilimo kuwa kiwanda cha uzalishaji.

0 comments:

Post a Comment