Kwa mara ya kwanza Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, atazuru taifa jirani la Kenya hapo kesho Jumatatu.
Ziara ya Magufuli nchini humo, inatukia wakati ambapo uhusiano wa mataifa hayo mawili umekuwa ukilegea.
Kwenye ajenda ya ziara hiyo rasmi ya kiserikali, kati yake na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, ni kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili, kwani Rais magufuli amekosa kuhudhuria mikitano mikuu miwili jijini Nairobi, iliyowaleta pamoja marais wengi wa Afrika.
Tangu aingie mamlakani mwezi Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli ambaye ameamua kukabiliana na ufisadi nchini mwake amezuru tu Rwanda na Uganda.
Pia ziara ya Dkt Magufuli inahusia na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kumpendekeza waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed kwa kinyanganyiro cha wadhifa wa mwenyekiti wa muungano wa afrika-AU.
Tofauti na Tanzania, kashfa za mamilioni ya dola inafichuliwa mara kwa mara nchini Kenya, huku pesa za umma zikinyakuliwa na baadhi ya watu mashuhuri serikalini na walio na uhusiano wa karibu na watawala wa nchi hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta atamkaribisha mgeni wake jijini Nairobi, baada ya Kenyatta kukamilisha ziara ya siku mbili huko Khartoum, alipokutana na Rais wa Sudan- Omar Al- Bashir.
Latest News
Loading...
Home »
KITAIFA
» Kwa Mara ya Kwanza Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli Kutembelea Nchini Kenya....
Kwa Mara ya Kwanza Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli Kutembelea Nchini Kenya....
Related Posts:
Umoja wa Ulaya (EU) Waweka Rehani trilioni 2.182 za Tanzania.......Wabunge wa Uingereza Wataka Serikali Yao Ikate Misaada Tanzania Siku chache baada ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), kufuta Tanzania kwenye nchi wanachama wake na hivyo kuikosesha serikali msaada wa zaidi ya Sh. trilioni moja kutokana na uchaguzi wa Zanzibar, Umoja wa Ulaya (EU)… Read More
Freeman Mbowe, Halipwi Mshahara Wowote na Chama Wala Posho Baada ya wengi sana jana kuhoji mshahara wa mwenyekiti wa chadema .mh freeman mbowe kufuati mh rais kutaja mshara wake. HILI NDIO JIBU LAKEMwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe halipwi mshahara wowote na Chama. Amekitum… Read More
Aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Mkoa wa Mwanza Ajivua Uanachama Aliyekuwa Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mwanza, Adrian Tizeba ametangaza kujivua uanchama na kuachana na siasa. Tizeba aliyesimamishwa uongozi na Baraza la Uongozi la Chadema tangu Me… Read More
Kaya 40 Zakosa Makazi baada ya nyumba zao kubomolewa na Mafuriko ya Mvua Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi imeleta athari kubwa katika Kijiji cha Chenene Kata ya Haneti Tarafa ya Itiso, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kukosesha makazi zaidi ya kaya 40. Akizungumza jan… Read More
GARI Lateketea Kwa Moto Pamoja na Dereva Akiwa Ndani.. KUNA GARI IMEPATA AJALI MAENEO YA MBEZI BEACH AFRICANA GARI NO T598BEL TOYOTA LANDCRUISER DEREVA KAUNGUA HAJAFAHAMIKA HATA KWA SURA,SAMBAZA UJUMBE HUU GROUP TOFAUTI ILI WENYE NDUGU WAMFAHAMU,GARI LIPO POLISI KAWE. … Read More
0 comments:
Post a Comment