Latest News
Loading...

Breaking News: Rais Magufuli Amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe

Rais Magufuli amemsimamisha kazi mchana huu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe kutokana na ufisadi wa kutisha katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji  na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  bilioni 3.

Rais Magufuli amechukua uamuzi huo mchana huu wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda alitoa Hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo.

Akieleza zaidi, Makonda  amesema, Kamati aliyounda  ilibaini kuwa pale ubungo kunatumika sheria ndogo mbili za ukusanyaji mapato moja ya mwaka 2004 na nyingine ya mwaka 2009  ambazo zote zilisainiwa na Wilson Kabwe.

Amesema  kuwa Sheria  ya Mwaka 2004 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila basi  linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 4,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa kituoni hapo   na   Sheria  ya Mwaka 2009 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila basi  linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 8,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 82  kwa mwezi

Makonda amesema kwamba, Kabwe alisaini mikataba miwili, wa 2004 na wa mwaka 2009  ambapo ule wa mwaka 2004  ulipelekwa jiji  na  ule wa 2009 ukapelekwa kwa mzabuni, hivyo jiji wanajua kuwa basi linatozwa sh. 4000 kwa  siku wakati mzabuni  anatozwa  8000 kwa siku

Kutokana  na  maelezo hayo, Mheshimiwa Rais ametangaza kumsimamisha kazi bwana Kabwe ambaye  ni  Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam  na ameagiza vyombo vya dola vianze uchunguzi mara moja ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa

0 comments:

Post a Comment