Hatimaye mkutano wa kwanza kikao cha 3 wa bunge umeanza leo kwa wabunge kuimba wimbo wa taifa na baadhi yao kula kiapo. Tazama kilichoendelea leo.
Je ni nini hatma ya uchaguzi kwa majimbo ya Bulyankulu na kamindo ikiwa uchaguzi haujafanyika hadi leo? Dkt. Abdallah Possy atoa ufafanuzi.
Mhe. Suleiman Jafo atoa ufafanuzi na utaratibu wa serikali juu ya hospitali zinazopandishwa hadhi kukidhi haja za wananchi.
Mbunge wa Njombe mjini aihoji serikali juu ya upigaji marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki unaosababisha uharibifu wa mazingira.
Naibu waziri wa nishati na madini Dkt Medard kalemani atoa ufafanuzi wa kuanza kwa mradi wa kuzalisha umeme wa Malagarasi.
Je serikali inaweka msukumo gani kwa Geita Gold Mining kuhakikisha inawalipa wananchi wa mtaa wa Mgusu fidia ili kupisha eneo hilo?
Kauli ya Wizara ya mambo ya ndani kuhusu baadhi ya vituo vya polisi nchini kuwa na askari wachache na kutofanya kazi kwa masaa 24.
Je ni lini uwanja wa ndege wa Musoma utajengwa na kuwa kwenye hadhi ya stahiki ya kitaifa au kimataifa? Mhe. Joyce Sokombi ahoji.
0 comments:
Post a Comment