Ile Vuta N’kuvute ya vituo vya redio inaendelea na sasa East Africa Radio imekuwa mhanga mpya.
Dj wa kike, Sinyorita na mtangazaji wa The Cruise, Mami wanadaiwa kuondoka East Africa Radio kuanzia wiki hii baada ya kupata dau kubwa kutoka kwa guess what? Clouds FM.
Tetesi hizo zilianza kuvuma tangu wiki iliyopita lakini jana zimeonekana kupata ukweli baada ya wawili hao kutosikika kwenye kipindi cha The Cruise, kitu ambacho si cha kawaida.
Tetesi zinadai kuwa tangu Dj Fetty aache kazi Clouds FM, wamekuwa wakitafuta mtangazaji wa kike anayeweza kuchukua nafasi yake na Mami anaonesha kuwa na caliber hiyo.
Tayari wawili hao wamebadilisha profile zao za Instagram kwa kuondoa kipengele cha kuwa ni wafanyakazi wa East Africa Radio.
Latest News
Loading...
Home »
KITAIFA
» Clouds FM Yaendeleza Nyakua Nyakua ya Watangazaji na Madj..Wamewachukua Hawa East Africa Radio
Clouds FM Yaendeleza Nyakua Nyakua ya Watangazaji na Madj..Wamewachukua Hawa East Africa Radio
Related Posts:
Tanzania Na Burundi Zatakiwa Kulegeza Msimamo Ndani Ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) Tanzania na Burundi zimeombwa kulegeza misimamo yao kwa kuondoa gharama za vibali vya kufanya kazi kwa raia wa nchi zinazounda jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kama zilivyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya ambaz… Read More
Tamko la Serikali kuhusu kutatua Kero na Changamoto za Sekta ya Usafirishaji Barabarani Ikiwemo Kuyaondoa Matuta Yote Barabarani 1.0 Mnamo tarehe 09/4/2015 ulifanyika mgomo wa madereva nchini uliohusu malalamiko na kero mbalimbali za madereva. Katika kuzipatia ufumbuzi kero hizi, &nbs… Read More
Wabunge Washtushwa TCRA kutumia Bilioni 18 kwa Semina na Warsha Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji (PIC) imeshtushwa baada ya kubaini Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitumia Sh18 bilioni mwaka 2013/2014 kwa ajili ya mafunzo, semina na warsha. Makamu mwenyekiti wa kama… Read More
Kamati ya Bunge Yaingilia kati Madaktari kutumbuliwa Majipu Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imelaani wanasiasa wanaoingilia utendaji katika Sekta ya Afya kwa kutoa adhabu kwa madaktari na wauguzi, bila kushirikisha vyombo vyao. Wakizungumza katika Hospitali ya… Read More
Mafuriko yafunga Barabara kuu Itokayo Dodoma Kwenda Morogoro kwa saa 10 Zaidi ya magari 1,500 jana, yalikwama katika eneo la Chalinze Nyama wilayani Chamwino mkoani Dodoma kwa zaidi ya saa 10, baada ya mafuriko kuziba barabara kuu itokayo Dodoma kwenda Morogoro. Mafuriko hayo yalitokana … Read More
0 comments:
Post a Comment