Habari zilizolifikia Wikienda mara tu baada ya kutokea kwa msiba huo asubuhi ya Jumamosi iliyopita zilieleza kuwa, Ndanda alisumbuliwa na tumbo ambapo alilazwa kwenye Hospitali ya Mwananyama na baadaye kuhamishiwa Muhimbili jijini Dar.
Akizungumza na Wikienda, mjomba wa Ndanda ambaye pia ni mwanamuziki, Cardinal Gento alisema kuwa, Ndanda alihamishiwa Muhimbili baada ya tatizo lake kushindikana Mwananyamala.
“Nilikesha naye hospitalini, ilipofika asubuhi nikaondoka kurudi nyumbani kwa ajili ya chakula, nikaacha anafanyiwa mpango wa damu maana alikuwa amepungukiwa, lakini muda mfupi baada ya kuondoka, nikapigiwa simu amefariki dunia,” alisema Gento wakiendelea na utaratibu wa msiba nyumbani kwa Ndanda, Madale, Dar.
Kabla ya kukutwa na umauti, historia ya ugonjwa wake inaonesha ilianza mwaka jana ambapo aliripotiwa na Magazeti ya Global kuwa alilazwa kwenye Hospitali ya PKA iliyoko Tegeta, Dar akisumbuliwa na tatizo la kupasuka kwa mmoja wa mishipa tumboni hivyo kutapika damu.
HISTORIA FUPI YA NDANDA KOSOVO
Ndanda aliwika na Bendi ya FM Academia International ambapo alitunga nyimbo za FM Academia baada ya kutoka jela akiwa na akina Nyoshi El-Sadaat, Maluu Stonch, Mulemule FBI, King Blaize, Patcho Mwamba, Gento na wengine kibao waliotamba na Wimbo wa Wajelajela.
Baadaye Ndanda alitoka FM Academia International akaanzisha Bendi ya Stono Musica akiita Wajelajela Original akiwa na Maluu, Chai Jaba, Patcho na wengine. Miongoni mwa nyimbo zake zilizotamba ni pamoja na Binadamu pamoja na rap zake za Kidedea na Kaokota Big G.
Baadaye Ndanda aliachana na Stono Musica akaelekea Marekani kwa shughuli za kimuziki ambazo zilikuwa na mafaniko makubwa. Aliporejea Bongo ndipo akaanzisha Kundi la Watoto wa Tembo kabla ya kuachana na bendi na vikundi na kuwa msanii anayejitegemea.
Chanzo:GPL
Latest News
Loading...
Undani Kifo cha Mwanamuziki Ndanda Kosovo Huu Hapa...
Related Posts:
Hatimaye Msanii Ney wa mitego kasalimu amri Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego ameanza kutekeleza baadhi ya maagizo aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa baada ya kufungiwa kwa wimbo wake wa ‘Pale Kati’. Rapper huyo alipewa adhabu hiyo pamoja na kulipa fain… Read More
Chris Brown Akiri Alitaka Kujiua Kwa Sababu ya Penzi la Rihanna Chris Brown amesema alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.Katika kipande kifupi cha makala yake ya ‘Karibu katika maisha yangu’,mwanamuziki huyo wa mtindo wa R &… Read More
Video;Itazame Historia Zari The Boss Lady Pamoja na Utajili Wake. Je unamjua Vizuri Zari Hassan Mama Mtoto wa Mwanamuziki Diamond Platnumz?Video hii Hapa chini itakupa kujua Zari ni Nani pamoja na thamani ya utajiri wakeTazama Video: … Read More
Music: Christian Bella – Nishike Mfalme wa masauti Christian Bella baada ya kuachia video ya wimbo “Nishike”, Hii ni Audio ya wimbo huo. Producer Abby Dad. … Read More
Harmonize Afungukia Maumivu ya Mahusiano, Amshangaa Diamond Msanii wa bongo flava Harmonize anayetamba na wimbo “Bado’ ameshangazwa na namna ambavyo Msanii Diamond Platnumz anavyoweza kuhimili maumivu ya kimapenzi. Akizungumza katika kipindi enewz cha EATV amesema kuwa … Read More
0 comments:
Post a Comment