Latest News
Loading...
Showing posts with label WASANI. Show all posts
Showing posts with label WASANI. Show all posts

Picha: Show ya Diamond Malawi yafana licha ya mvua kubwa kunyesha

Licha ya mvua kubwa kunyesha, Diamond amefanikiwa kupiga show iliyofana kwenye Sand Music Festival iliyofanyika kwenye fukwe za Living stone Jumamosi hii.
14717487_1627203447579395_8916577059703095296_n
Mpiga picha wake, Kifesi amedai kuwa mvua kubwa ilinyesha na kulazimu show yake kusimama kwa muda. Hata hivyo mashabiki waliokuwa na hamu kumuona akitumbuiza, walisubiri hadi ilipokata.
14718155_570664783139840_4137945881523519488_n
Kwenye picha hii Kifesi ameandika: Picha juu ni usiku watu wakiwa na shauku ya Diamond but mvua ikanyesha, but walingoja hadi hali ilipotulia.. Picha chini na alfajiri saa 12 hali ilipotulia na Diamond kupanda na hakuna alokua kuchoka or kuondoka
Kwenye show hiyo Diamond alitumbuiza live. Hizi ni picha zaidi:

14583435_409418349445961_5204304046856339456_n

14624250_155985254866483_6975121932035293184_n

14624485_1894274970800430_379055413905063936_n

14624792_324952597861913_6656501196225773568_n

14677395_1800999240140394_6583553105143529472_n

14704955_1271863276168130_6216880717607993344_n

14712335_574537479402409_7144748499999916032_n

14712409_1655487558074513_6202943742006001664_n

14716485_557850674403755_8102136125193191424_n

14718136_311628412557770_2527903349676703744_n

14718276_1675009502829719_636843465589653504_n
14723446_905749922891304_4656700565634416640_n

Kadjanito adai ndoa haitomtenganisha na muziki

Msanii wa Bongo Flava, Khadija Said Maige, maarufu kama Kadjanito amesema licha ya kufunga ndoa, muziki ataendelea kuufanya kama kawaida. Muimbaji huyo atafunga ndoa na mchezaji wa mpira, Tresor Lisimo, Jumamosi hii, Oktoba 29.
kadjanito
Akiongea kupitia E-Newz, Kadja amesema aliona amekaa kwa muda mrefu peke yake hivyo ameamua kuwa mke wa mtu.
“Nimeamua kufunga ndoa kwani nilikaa muda mrefu peke yangu nikatafakari nikaona siyo kitu kizuri nikiwa kama msichana ambaye nina ‘Inspire’ watu wengi lazima kuna vitu nifanye ili niwe mwanamke kamili, maana ukiwa peke yako mtu anaweza kukuchukulia labda huyu mtu muhuni lakini mimi nimeamua kuwa mke wa mtu. Najua ni kitu kikubwa lakini haitanifanya mimi niache kazi zangu za muziki,” alisema.
“Nimeamua kufunga ndoa sababu nimeona nimepata mtu ambaye tunapendana, ninaendana naye na ninampenda sana.”
Licha ya kuwa muislamu, Kadja amesema atafunga ndoa ya Kikristu.

Video: Diamond awasili kwenye mjengo wake wa SA, awapa madongo waliosema si wake

Afrika Kusini sasa imekuwa nyumbani kwingine kwa Diamond baada ya kununua nyumba ya kifahari iliyopo jijini Pretoria.
diamond
Baada ya kutangaza kununua nyumba hiyo iliyomgharimu zaidi ya shilingi milioni 400, maneno mengi yalisemwa yakiwemo ya wale waliohisi amepiga changa la macho. Na sasa muimbaji huyo amethibitisha kuwa mjengo huo ni mali yake baada ya kuwasili rasmi Jumanne hii.
Akiwa na timu yake ya WCB, Diamond ameikagua nyumba kwa mara ya kwanza na kuwasogeza karibu nayo mashabiki wake kwa video alizoweka Instagram.
“Meet my neighbors ðŸ˜Š…mnh ujirani huu hata siku Ukiwa na shida ya chumvi sjui unaingiaje kujichekesha upewe!…. #MyNewCribInSouthAfrica,” ameandika kwenye video moja.
Kwenye nyingine ameandika, “Wow! If you don’t know yet today was my first time seeing my house physically since I bought it a month ago….and honestly I went crazy when I saw it coz I was so excited to… so proud of my baby @zarithebosslady for being a good leader in our love and life..”
Ya mwisho ilikuwa na ujumbe mkali zaidi uliowalenga wale waliodai si nyumba yake.
“Asa k*nya nak*nya mie makalio yanawauma wengine, eti inahuu..,” ameandika.
“Wambie wasininunie mie, wakazane….halaf hii clip naomba wanangu mnisaidie kuwatag wote waliokuwa busy kupost na kuzungumza Kuwa nyumba hii si yangu….waambie hizi ndio kwanza rasharasha clip hata kupost sijaanza bado..”
“Soon naamia ndani😂😂…halaf nlisahau, wakikwambia mie mswahili wambie Mswahili haswaaa👌… halaf uswahili wangu najua kuutumia na umefanya leo niwe na kibanda south asa wao Uzungu wao Umewapa nini?”

Music: Masai Wa Kigoma – Sinasi

sinasi
Msanii Masai wa Kigoma kama anavyo jiita ameachia wimbo mpya unaitwa “Sinasi”. Huu ni wimbo ambao upo katika maadhi ya muziki wa Singeli sikiliza hapa.


Diamond, Alikiba, Vanessa, Navy Kenzo, AY watajwa kuwania tuzo za WatsUp TV Ghana

Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee, Navy Kenzo, AY, Mayunga, Harmonize na Ray Vanny wametajwa kuwania tuzo zaWatsUp TV Africa Music Video Awards – WAMVA16 za Ghana.
tuzo
Hivi ndio vipengele ambavyo wasanii wa Tanzania wametajwa:
African Video Of The Year
Diamond ft P-Square – Kidogo
Best African RnB Video
AliKiba – Aje
Best African Performance
Diamond – Jembeka Festival

Best African Group/Duo Video

Navy Kenzo – Kamatia
Best African New Comer Video
Mayungaa ft Akon – “Please Don’t Go Away”
Harmonize ft Diamond – Bado
Best African Reggae/Dancehall
Navy Kenzo – Kamatia
Best East African Video 
Alikiba – Aje
Ray Vanny – Kwetu
Navy Kenzo – Kamatia
Harmonize ft Diamond – Bado
AY f. Diamond – Zigo Remix
Diamond ft P-Square – Kidogo
Best African Female Video
Vanessa Mdee – Niroge
Best African Male Video
Diamond ft P-Square – Kidogo
Best African Combo Video
Diamond ft AKA – Make Me Sing

VIDEO: Diamond Platnumz ametaja gharama alizonunulia Nyumba South Afrika


September 23 2016 Diamond Platnumz aliingia kwenye headlines baada ya kupost Nyumba ambayo aliandika kuwa ni zawadi kuwa Mpenzi wake ambaye ni Mrembo Zari, Baada ya Diamond Platnumz kupost Nyumba hiyo ambayo iko South Africa zimepita  siku saba na amehojiwa na kipindi cha Weekend Chat Show na kazitaja Gharama alizonunulia Nyumba hiyo.


Kuna matumaini Daniel Craig akaendelea kuigiza kama James Bond

Watayarishaji wa filamu wana matumaini kuwa Daniel Craig ataendelea kucheza filamu hizo.
spectre-spectre-onesheet
Daniel alidaiwa kutotaka kuendelea tena na mradi huo na hivyo kuwepo tetesi za waigizaji wengine kuchukua nafasi yake kama James Bond. Kwa mujibu wa mmoja wa watayarishaji wa filamu hizo, Daniel bado anakubalika zaidi kuendeleza uhusika wa 007.
Callum McDougall, aliyefanya kazi kwenye filamu zote za Bond kuanzia Die Another Day, alisema kuwa Craig ni chaguo la kwanza la watayarishaji wakuu, ambani ni ndugu, Barbara Broccoli na Michael G. Wilson.
“Najua wana matumaini kuwa atarejea,” alisema kwenye mahojiano na BBC.
Inadaiwa kuwa Craig alikataa dau la $99m kuigiza kwenye filamu mbili mpya za Bond.
Kwa sasa waigizaji wanaopigiwa debe kushika nafasi hiyo ni Idris Elba, Tom Hiddleston na Aiden Turner.

Yemi Alade akiishi alichokifanya Michael Jackson, Brazil

Staa wa Nigeria, Yemi Alade ametumia location iliyopo nchni Brazil kwenye mji wa Rio de Jeneiro ya Favela of Dona Marta aliyowahi kuitumia mfalme wa muziki wa pop duniani, marehemu Michael Jackson kwenye video ya wimbo wake wa ‘The Don’t Care About Us.’
yemi-alade-brazil-10-600x400
Yemi yupo nchini humo kwaajili ya mradi wa kampuni ya mafuta ya Shell, uliopewa jina ‘Make The Future’ akiungana na mastaa wengine wakubwa wakiwemo Jennifer Hudson, Pixie Lott, Steve Aoki, Tan Wei Wei na Luan Santana.
yemi-696x661
yemi-alade-brazil-4-600x400
yemi-alade-brazil-5-600x900
yemi-alade-brazil-12-600x400
yemi-alade-brazil-13-600x400
yemi-alade-brazil-1-600x400
yemi-alade-brazil-2-600x400
yemi-alade-brazil-3-600x400
Hata hivyo Michael Jackson alikutana na wakati mgumu kutoka kwa serikali ya Brazil kutokana na kuzuiwa kushoot video yake kwenye eneo hilo kwakuwa kipindi hicho mji wa Rio haukuwa mkubwa na waliamini hautaitangaza nchi yao vizuri.
yemi-alade-brazil-6-600x400

Mke wa mtu amponza Tunda Man

Msanii wa Tip Top Connection, Tunda Man ameshindwa kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Mwanaume Suruali’ baada ya kumtumia mke wa mtu kama video queen.
tundamantz
Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo ‘Mama Kijacho’, ameiambia Bongo5 kuwa ameshindwa kuachia kazi hiyo kutokana na mume wa mwanamke huyo kuzuia video hiyo sitoke.
“Kuna video ya wimbo wangu mpya ‘Mwanaume Suruali’ ambayo ilikuwa itoke hivi karibuni lakini kwa bahati mbaya mume wa video queen ambaye ametumika kwenye video amezuia video isitoke,” alisema Tunda. “Kwa hiyo bado tupo kwenye mazungumzo, kama akiruhusu itoke video itatoka hivi karibuni,”
Akifafanua zaidi kilichotokea Tunda alisema “Mimi nilikuwa nipo Dar nilimwachia mtu kazi Zanzibar ya kutafuta location na mambo mengine, kwa hiyo kwa bahati mbaya au nzuri akampata mwanamke ambaye na mimi nilipenda aonekane kwenye video. Kweli tukafanya naye video na pesa yake akalipwa, lakini mwanamke hakusema kama yeye ni mke wa mtu, kwa hiyo baada video kumalizika zile picha za behind the scene mume wake akaziona ndo akaamua kutushtaki ili video isitoke. Lakini tunashukuru mungu mambo yanaenda vizuri soon mambo yakienda kama yalivyopanga ngoma itatoka,”

Mama Diamond ampongeza Wema kwenye birthday yake baada ya kumkaushia Zari

Mama Diamond, Bi Kendrah, amemtonesha mchumba wa mwanae, Zari pale panapomuuma zaidi.
ddss
Amempongeza ex wa Diamond, Wema Sepetu katika birthday yake, Jumatano hii, Septemba 28, siku chache tu baada ya kumkaushia Zari kwenye birthday yake – ajabu!
Happy birthday.. Mamy akee @wemasepetu mungu akuongezee umri na akujali kheri akufungulie Mlango wa baraka kwa kila uliombalo.Amin😘😘 ðŸ‘‘🎉🎊,” ameandika Bi. Kendrah Jumatano hii.
Post hiyo inadhihirisha uvumi wa muda mrefu kuwa Zari haelewani na mama mkwe wake huyo pamoja na ndugeze wengine wake Diamond. Wifi yake, Esma naye alimkaushia raia huyo wa Uganda mwenye makazi yake Afrika Kusini.
c
Kwa muda sasa Zari na mama mkwe wake hawana maelewano mazuri
Minong’ono inadai kuwa Zari hakubaliki ukweni kutokana na kupenda maisha ya kizungu, kutawala mipango ya Diamond na huenda ndio chanzo cha Bi Kendrah kuondoka Madale, nyumbani kwa staa huyo.
Pamoja na Zari kutokubalika ukweli, Diamond haoneshi kushtushwa na hali hiyo kwakuwa hivi karibuni alimzawadia nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 396 ya Afrika Kusini pamoja na kumpeleka visiwani Zanzibar kusherehekea birthday yake.
14478283_1754239714834549_1107689331406929920_n
Labda ndugu za Diamond inabidi waukubali tu ukweli mchungu kuwa Zari sasa ndio kila kitu kwa staa huyo. Wakiwa na mtoto mmoja sasa, Tiffah, wawili hao wanatarajia kuongeza mtoto wa pili December mwaka huu.

Video: Motra The Future Ft. Ruby – One Day

Rapper Montra ameachia video mpya ya wimbo ambao unaitwa “One Day”, amemshirikisha Mwanadada Ruby. Video imeongozwa na Pascal Katambo.


Aunt Ezekiel awajibu wanaodai anajipendekeza kwa Zari ‘kwani yule si bosi wa mkata viuno wangu’

Malkia wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Aunt Ezekiel amewamind mashabiki katika mitandao ya kijamii ambao wanadai anajipendekeza kwa mama watoto wa Diamond, Zari, baada ya hivi karibuni kuonekana akila nao bata pamoja.
14310603_158656564586124_2312098998447505408_n
Mwingizaji huyo ambaye alikuwa rafiki wa Wema Sepetu, amesema lazima awe karibu na familia ya bosi wa mume wake kwa kuwa hao ndio waliomwajiri mume wake.
“Nataka niwaambie kitu kimoja maana kujibu mmoja mmoja muda huo sina ni hivi nafanya nitakalo sifanyi mtakayo, maana nina uhakika nyie mnaokaa kubishana na mimi vibanda vya mbavu za mbwa vinawashinda, so muda mnaokaa mkafatilia yangu mngeenda kutafuta yakufanya, ooh! njaa yes i say tena yes maana mnataka nibadili red kuwa yellow kwani yule si ni boss wa mkata viuno wangu au!. Sasa kama ni bosi ulitaka nibishe niseme mimi ndio bosi, basi nifungue bendi yetu acheze!,” Aunt Ezekiel aliandika instagram.
Aliongeza, “Mnawazimu nini na namweshimu kama mshkaji rafiki bosi wa bwana yangu na siwezi acha kushirikiana na familia yake eti kisa ushuzi mtasema nini. Sitaki kutaja majina ya watu ila kilichopo ndio ukweli asilia, Mama Tee ndio mwanamke na mama watoto wa Nasibu no way hata tulambe lami kubadili ni ngumu ila mwenyewe akibadili basi na sisi tutabadili ila kwa sasa ni Mama tee shukrani gud Day,”.
Mwigizaji huyo anatoka kimapenzi na densa wa Diamond, Mose Iyobo ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kupata mtoto mmoja aitwae Cookie.

Chris Brown na Wizkid kutumbuiza Mombasa, Oktoba 8

Chris Brown na Wizkid wanatarajiwa kutumbuiza pamoja kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music Festival nchini Kenya, Oktoba 8, mwaka huu.
chris
Hiyo itakuwa si mara ya kwanza kwa wasanii hao kutumbuiza pamoja kwani mwezi Juni, mwaka huu walitumbuiza pamoja kwenye show ya ziara ya One Hell of a Nite Tour 2016 ya Chris Brown huko Uingereza na Amsterdam.
chris-brown-x-wizkid-african-bad-girl
Mwaka huu umekuwa ni wa mafanikio kwenye muziki wa Wizkid kutokana na kuonekana kuwa karibu na mastaa wakubwa duniani huku akishirikishwa kwenye nyimbo zao akiwemo Drake, Justine Skye, Chris Brown, Tenie Tempah na Swizz Beatz

Picha: Diamond na Zari waendeleza bata lao Zanzibar

Zanzibar kwa wenye fedha zao huweza kugeuka kuwa paradise iliyo chini ya jua. Kwa Diamond, Zanzibar imekuwa ni sehemu muhimu pindi anapotaka kumpeleka mapumzikoni mchumba wake, Zari.
14482765_325944324422569_2369523093447114752_n
Kwa dhoruba kadhaa zilizojaribu kulipiga pendo lao miezi ya hivi karibuni, mapumziko katika fukwe za visiwani humo zenye ukijani unaovutia na upepo mwanana wa bahari ya Hindi, kilikuwa ni kitu walichokihitaji zaidi.
14350800_655042867993320_3104029343639142400_n
Isitoshe, Zari amesherehekea siku yake ya kuzaliwa siku mbili hizi – siku ambayo imemkuta akiwa amejaa, mimba nyingine, ya mtoto mwingine wa kipenzi chake, Diamond. Ni zawadi gani nyingine alipaswa kupewa na mpenzi wake zaidi ya kupelekwa kwenye kisiwa hicho cha karafuu?
14359462_1289578727752813_8255799012683153408_n
Nguo nyeupe likawa chaguo lao na picha zao zilizopigwa nyumba ya mazingira ya kuvutia ya Zanzibar, zimeng’aa haswaa. Chini ni baadhi ya picha hizo.

14449152_1807308329504796_7769537358189297664_n

14310603_158656564586124_2312098998447505408_n

14350702_1777066919202678_5949122388972011520_n

14350865_984556874986808_2455024042495705088_n

14350964_662324507258812_4907645785228705792_n

14369077_961752607287190_3769994207914098688_n
14374212_1773272106292175_1753673247611682816_n