Latest News
Loading...

Kadjanito adai ndoa haitomtenganisha na muziki

Msanii wa Bongo Flava, Khadija Said Maige, maarufu kama Kadjanito amesema licha ya kufunga ndoa, muziki ataendelea kuufanya kama kawaida. Muimbaji huyo atafunga ndoa na mchezaji wa mpira, Tresor Lisimo, Jumamosi hii, Oktoba 29.
kadjanito
Akiongea kupitia E-Newz, Kadja amesema aliona amekaa kwa muda mrefu peke yake hivyo ameamua kuwa mke wa mtu.
“Nimeamua kufunga ndoa kwani nilikaa muda mrefu peke yangu nikatafakari nikaona siyo kitu kizuri nikiwa kama msichana ambaye nina ‘Inspire’ watu wengi lazima kuna vitu nifanye ili niwe mwanamke kamili, maana ukiwa peke yako mtu anaweza kukuchukulia labda huyu mtu muhuni lakini mimi nimeamua kuwa mke wa mtu. Najua ni kitu kikubwa lakini haitanifanya mimi niache kazi zangu za muziki,” alisema.
“Nimeamua kufunga ndoa sababu nimeona nimepata mtu ambaye tunapendana, ninaendana naye na ninampenda sana.”
Licha ya kuwa muislamu, Kadja amesema atafunga ndoa ya Kikristu.

0 comments:

Post a Comment