Zanzibar kwa wenye fedha zao huweza kugeuka kuwa paradise iliyo chini ya jua. Kwa Diamond, Zanzibar imekuwa ni sehemu muhimu pindi anapotaka kumpeleka mapumzikoni mchumba wake, Zari.
Kwa dhoruba kadhaa zilizojaribu kulipiga pendo lao miezi ya hivi karibuni, mapumziko katika fukwe za visiwani humo zenye ukijani unaovutia na upepo mwanana wa bahari ya Hindi, kilikuwa ni kitu walichokihitaji zaidi.
Isitoshe, Zari amesherehekea siku yake ya kuzaliwa siku mbili hizi – siku ambayo imemkuta akiwa amejaa, mimba nyingine, ya mtoto mwingine wa kipenzi chake, Diamond. Ni zawadi gani nyingine alipaswa kupewa na mpenzi wake zaidi ya kupelekwa kwenye kisiwa hicho cha karafuu?
Nguo nyeupe likawa chaguo lao na picha zao zilizopigwa nyumba ya mazingira ya kuvutia ya Zanzibar, zimeng’aa haswaa. Chini ni baadhi ya picha hizo.
0 comments:
Post a Comment