Watayarishaji wa filamu wana matumaini kuwa Daniel Craig ataendelea kucheza filamu hizo.
Daniel alidaiwa kutotaka kuendelea tena na mradi huo na hivyo kuwepo tetesi za waigizaji wengine kuchukua nafasi yake kama James Bond. Kwa mujibu wa mmoja wa watayarishaji wa filamu hizo, Daniel bado anakubalika zaidi kuendeleza uhusika wa 007.
Callum McDougall, aliyefanya kazi kwenye filamu zote za Bond kuanzia Die Another Day, alisema kuwa Craig ni chaguo la kwanza la watayarishaji wakuu, ambani ni ndugu, Barbara Broccoli na Michael G. Wilson.
“Najua wana matumaini kuwa atarejea,” alisema kwenye mahojiano na BBC.
Inadaiwa kuwa Craig alikataa dau la $99m kuigiza kwenye filamu mbili mpya za Bond.
Kwa sasa waigizaji wanaopigiwa debe kushika nafasi hiyo ni Idris Elba, Tom Hiddleston na Aiden Turner.
0 comments:
Post a Comment