Staa wa Nigeria, Yemi Alade ametumia location iliyopo nchni Brazil kwenye mji wa Rio de Jeneiro ya Favela of Dona Marta aliyowahi kuitumia mfalme wa muziki wa pop duniani, marehemu Michael Jackson kwenye video ya wimbo wake wa ‘The Don’t Care About Us.’
Yemi yupo nchini humo kwaajili ya mradi wa kampuni ya mafuta ya Shell, uliopewa jina ‘Make The Future’ akiungana na mastaa wengine wakubwa wakiwemo Jennifer Hudson, Pixie Lott, Steve Aoki, Tan Wei Wei na Luan Santana.
Hata hivyo Michael Jackson alikutana na wakati mgumu kutoka kwa serikali ya Brazil kutokana na kuzuiwa kushoot video yake kwenye eneo hilo kwakuwa kipindi hicho mji wa Rio haukuwa mkubwa na waliamini hautaitangaza nchi yao vizuri.
0 comments:
Post a Comment