Latest News
Loading...

Manji aizawadiwa Yanga ekari 715 zijengwe uwanja wa kisasa maeneo ya Kigamboni

Hatimaye klabu ya Yanga imepata sehemu nyingine ya kujenga Uwanja wa kisasa kutoka kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yussuf Manji ametoa eneo la ekari 715 na kuikabidhi klabu hiyo maeneo ya Kigamboni Geza Ulole jijini Dar es Salaam maalum kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na wa klabu hiyo.
img-20160928-wa0045
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Waziri wa Mambi ya Ndani, Mwigulu Nchemba, mke wa rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Sheikh Abeid Amaan Karume, Mama Fatma Karume ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo, ndiye aliyepokea eneo hilo.
img-20160928-wa0039
img-20160928-wa0041
yanga-na-manji-559x520
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mama Karume amesema wao kama Baraza la Wadhamini wanashukuru sana kupokea eneo hilo, kwani wanaamini ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti wao walipoketi kujdili suala hilo hatimaye imetimizwa.
Yanga wamepata eneo hilo huku mahasimu wao Simba wakiwa katika hatua za ujenzi wa uwanja wao uliopo Bunju.

0 comments:

Post a Comment