Latest News
Loading...

Idris Sultan aungana na Feza Kessy kama watangazaji wapya wa Choice FM

Idris Sultan ameungana na Feza Kessy kama watangazaji wapya wa Choice FM.

Wawili hao watakuwa wakitangaza kipindi cha Hard Drive kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa tatu.

“Wataelewa tuu @choicefmtz natanguliza shukrani kwa Mungu kisha tukutane saa 12 asubuhi mpaka saa 3 asubuhi. Ntawaamsha,” ameandika Idris.

Feza na Idris wamechukuliwa katika usajili mpya wa Clouds Media Group katika vituo vyake vya redio ambapo Clouds FM jana waliwatangaza rasmi Dj Sinyorita na Mami waliokuwa East Africa Radio kama wafanyakazi wao wapya.

0 comments:

Post a Comment