Rais wa Sudan Kusini Mhe. Jenerali Salva Kiir leo ametia saini mkataba wa nchi yake kujiunga rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Kiir ametia saini mkataba huo leo Jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Viongozi wa nchi za jumuiya hiyo waliidhinisha kukubaliwa kwa Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Arusha mwezi uliopita.
Sudan Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na Jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda kabla ya Rwanda na Burundi kujiunga na jumuiya hiyo baadaye.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa wakimsubiri Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016, Kushoto ni Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit akikagua gwaride la heshima wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu leo.
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir akiwapungia mikono viongozi mbalimbali huku akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakati alipowasili Ikulu
0 comments:
Post a Comment