Latest News
Loading...


Msimu Mpya Clouds FM
Mwezi huu umekuwa wa mapambano makubwa kati ya vituo vya redio viwili jijini Dar es Salaam, Clouds FM na EFM.

EFM walibomoa kipindi cha Power Breakfast kwa kuwachukua Gerald Hando, Paul James na mtayarishaji wa kipindi hicho, Abel Onesmo huku Clouds FM wakikibomoa kipindi cha Ubaoni cha EFM kwa kumchukua mtangazaji wake wa zamani, Gardener G Habash.

Gardener aka Captain anaanza kazi rasmi Jumatatu hii kwenye msimu mpya wa kituo hicho kwa kuendelea kukiendesha kipindi chake cha zamani, Jahazi.

Mtangazaji huyo anadaiwa kupewa mshahara mnono unaoweza kumfanya kuwa mtangazaji anayelipwa fedha nyingi zaidi kuliko wote Tanzania. Kwanza miongoni mwa vitu alivyopewa ili kurejea tena CMG ni gari aina ya Land Rover Discovery na mashavu mengine mengi.

Kwa upande wa EFM kuna kila dalili kuwa kipindi chao cha asubuhi kitapata nguvu mpya kuanzia wiki hii. Haijulikani ni watu wapi Clouds FM wamewachukua kuziba pengo lililoachwa kwenye Power Breakfast.

0 comments:

Post a Comment