Pazia la msimu mpya wa Sports Extra Ndondo Cup 2016 linafunguliwa leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye viwanja tofauti kukata utepe wa msimu mpya uliopewa kaulimbiu ya #Kampa Kampa Tena.
Uwanja wa Mwl. Nyerere upigwa mchezo kati ya Ubungo Bus Terminal dhidi ya Urafiki Shooting wakati kwenye uwanja wa Tanganyika Pakers utachezwa mchezo kati ya Kigoma United dhidi ya KISA FC.
Mratibu wa mashindano hayo Daud Kanuti amethibitisha kwamba kila kitu kiko sawa na michuano hiyo itaendelea kama ilivyopangwa, viongozi wa timu zote wametakiwa kufata ratiba kama inavyoelekeza na kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watapewa taarifa mapema.
Michuano ya Ndondo Cup imezidi kuchukua umaarufu jijini Dar es Salaam na imekuwa ikiwapa fursa wachezaji mbalimbali kuonekana na kupata timu ambazo zinashiriki ligi daraja la kwanza, daraja la pili pamoja na zile ligi za mikoa. Pia wajasiliamali wamekuwa wakifanya biashara kwa mashabiki wengi wanaojitokeza uwanjani kushuhudia game za Ndondo Cup.
Ikumbukwe kwamba, mabingwa watetezi wa michuano hiyo ni Faru Jeuri ambao waliibuka wababe wa kombe hilo mwaka 2015 na kujishindia kombe pamoja na pesa taslimu shilingi milioni tano (5,000,000).
0 comments:
Post a Comment