Latest News
Loading...

Video. Tazama FC Barcelona walivyokubali kipigo tena dhidi ya Valencia

April 17 2016 Ligi Kuu Hispania iliendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali, mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Valencia ndio ulikuwa wa kuvutia zaidi kwani mashabiki wa soka walikuwa wana hamu ya kufahamu kama FC Barcelona atakubali kipigo tena Nou Camp baada ya kufungwa na Madrid April 2.
Bado mambo sio mazuri kwa FC Barcelona leo April 17 2016 wamekubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Valencia katika uwanja wao wa Nou Camp, hivyo hilo ni pigo tena baada ya siku chache tu zimepita toka waondolewe katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya na klabu ya Atletico Madrid.
3347267600000578-0-image-a-1_1460921203091
Valencia walianza kufunga goli dakika ya 26 kupitia kwa mchezaji wa FC Barcelona Ivan Rakitic kujifunga, goli ambalo liliwafanya FC Barcelona kuhangaika kusawazisha ilaValencia wakafunga goli la pili dakika ya 45 kupitia kwa  Santi Mina ila Lionel Messidakika ya 63 aliipatia FC Barcelona goli la kufutia machozi.
Kwa matokeo hayo FC Barcelona ambao awali walikuwa wameziacha timu za Atletico Madrid na Real Madrid kwa point zaidi ya 5, wametoa nafasi ya nafasi ya kuwania Ubingwa kwa timu hizo kwani FC Barcelona anaongoza Ligi kwa tofauti ya magoli akiwa na point 76 sawa na Atletico, huku Real Madrid wakiwa na point 75.
Video ya magoli ya FC Barcelona vs Valencia, Full Time 1-2

0 comments:

Post a Comment