Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United Zlatan Ibrahimovic ni moja kati ya wanasoka au watu mashuhuri katika soka wanaoweza kuongea kauli zao za kujiamini kama ilivyo kwa kocha wake Jose Mourinho, Zlatan aliwahi kusema kuwa hakuna mchezaji anayeweza kukataa ofa ya kujiunga na Man United.
Kauli ambayo ilimfanya August 17 2016 mtandao wa 101greatgoals.com umletee list ya mastaa wa soka wa viwango vya dunia ambao wamewahi kuzipotezea ofa za kujiunga na Man United licha ya kuhitaji na klabu hiyo kwa zaidi ya mara moja.
List ya mastaa watano ambao wamewahi zipotezea ofa za kujiunga na Man United
1- Alan Shearer kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson amewahi kujaribu kutaka kumsajili Alan Shearer mara mbili wakati anaondoka Southampton na Blackburnlakini ilishindikana.
2- Usajili wa majira ya joto wa mwaka 2003 ulitawaliwa na jina la Ronaldinho ambaye alikuwa kamaliza mkataba wake na PSG, lakini ndio ilikuwa wakati wa David Beckhamanaondoka Man United, lakini Man United walishindwa kumpata Ronaldinho ambaye alinaswa na FC Barcelona.
3- Moja kati ya tetesi kubwa za usajili msimu uliopita ilikuwa ni Sergio Ramos kuhusishwa kwa karibu kujiunga na Man United akitokea Real Madrid, dili ambalo lilikatia njiani na hatimae staa huyo akaendelea na maisha yake ndani ya Real Madrid.
4- Katika kitabu cha maisha halisi ya kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Fergusonamekiri kuwa aliwahi kuhitaji huduma ya kiungo wa zamani wa Liverpool Steven Gerrardlakini mpango wake wa kumshawishi staa huyo ilishindikana.
5- Maisha ya Louis van Gaal ndani ya Old Trafford yalikuwa yakihusishwa kwa kiasi kikubwa na kusajili majina ya wachezaji wakubwa kutoka klabu yake ya zamani ya FC Bayern ya Ujerumani, licha Zlatan kuamini kuwa hakuna mchezaji anayeweza kukataa ofa ya kujiunga na Man United, Thomas Muller aliipotezea ofa ya Man United.
0 comments:
Post a Comment