Msanii wa muziki wa Pop Marekani, Lady Gaga amepata shavu la kuigiza kwenye filamu mpya ya ‘A Star Is Born’ akiwa kama mmoja wa mastaa kwenye filamu hiyo.
Hii itakuwa ni toleo jipya la filamu hiyo ambayo kwa mara ya kwanza ilifanyika mwaka 1954 lakini hapo awali nafasi hiyo ilipangwa kuchukuliwa na Beyonce. Mwigizaji Bradley Cooper anatajwa kuwa muongozaji huku Billy Gerber na Jon Peter wakiwa ndio watayarishaji wa filamu hiyo.
Mbali na kuigiza lakini pia Lady Gaga anatarajiwa kuandika na kuimba nyimbo mpya kwa ajili ya filamu hiyo. Filamu hiyo inatarajiwa kuanza kuchezwa kuanzia mwakani.
Lady Gaga anaungana na wasanii wengine wa Marekani waliopata shavu la kuigiza kwenye filamu tofauti akiwemo Mariah Carey, Rihanna na wengine wengi.
0 comments:
Post a Comment