Usiku wa Septemba 29 2016 klabu ya KRC Genk inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ilishuka uwanjani kucheza mchezo wake wa pili wa Kundi F wa Europa League dhidi ya Sassuolo ya Italia, Genk waliwakaribisha Sassuolo katika uwanja wao wa nyumbani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Rapid Wien.
Katika mchezo huo ambao KRC Genk waliingia kwa dhamira moja tu ya kupata point tatu, ulimalizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi mnono wa magoli 3-1, magoli ambayo yalifungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 8, mjamaica Leon Bailey dakika ya 25 naThomas Buffel dakika ya 61 wakati Sassuolo waliishia goli moja lililofungwa na Matteo Politano dakika ya 65.
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye alikuwa majeruhi aliingia dakika ya 75 kuchukua nafasi ya mgiriki Nikolaos Karelis aliyekuwa kwafunga goli la kwanza la Genk, ushindi huo wa KRC Genk unakuja ikiwa ni baada ya kukubali kipigo cha goli 3-2 katika mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Rapid Wien, Genk sasa watacheza mchezo wao wa tatu October 20 dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania.
0 comments:
Post a Comment