Tetemeko lingine baya la ardhi, limegonga maeneo ya katikati mwa Italia, mahali ambapo watu 300 waliuwawa mwezi Agosti mwaka huu.
Idara ya Seisomologia nchini Italia inakadiria kuwa tetemeko hilo lilikuwa lenye nguvu ya 6.5 katika vipimo vya Richa, tetemeko baya zaidi tangu lilile lililoitetemesha Italia mwaka 1980, iliyowauwa watu elfu 2,400.
Tetemeko la sasa limeporomosha jengo la kale la kanisa la mtakatifu Benedict mjini Norcia, pale wamonaki na watawa walikuwa wamekusanyika.
Meya wa mji ulioko karibu wa Ussita- Marco Rinaldi, amesema kuwa alikodolea macho kuzimu, kwani kila kitu kilichomzunguka kiliporomoka akitazama.
Duru zasema kuwa mji wa Amatrice -ambao uliharibiwa na tetemeko la mwezi Agosti, limeharibiwa tena zaidi.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kwamba watu tisa wamejeruhiwa lakini taarifa kuhusu vifo bado hazijatolewa.
Kitovu cha tetemeko hilo lilikuwa kusini mashariki mwa mji wa Perushia.
0 comments:
Post a Comment