Latest News
Loading...
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Tetemeko laporomosha majumba na kusababisha maafa makubwa.

Inasemekana kuwa watawa walinusurika kwa kukimbia kutoka ndani ya kanisa hili la mtakatifu Benedict mjini Norcia lililoporomokaImage copyright@MONKSOFNORCIA
Image captionInasemekana kuwa watawa walinusurika kwa kukimbia kutoka ndani ya kanisa hili la mtakatifu Benedict mjini Norcia lililoporomoka
Tetemeko lingine baya la ardhi, limegonga maeneo ya katikati mwa Italia, mahali ambapo watu 300 waliuwawa mwezi Agosti mwaka huu.
Idara ya Seisomologia nchini Italia inakadiria kuwa tetemeko hilo lilikuwa lenye nguvu ya 6.5 katika vipimo vya Richa, tetemeko baya zaidi tangu lilile lililoitetemesha Italia mwaka 1980, iliyowauwa watu elfu 2,400.
Majumba yaliyonusurika tetemeko la Julya sasa yameporomokaImage copyrightSABRINA FATAUZZI
Image captionMajumba yaliyonusurika tetemeko la Julya sasa yameporomoka
Tetemeko la sasa limeporomosha jengo la kale la kanisa la mtakatifu Benedict mjini Norcia, pale wamonaki na watawa walikuwa wamekusanyika.
Meya wa mji ulioko karibu wa Ussita- Marco Rinaldi, amesema kuwa alikodolea macho kuzimu, kwani kila kitu kilichomzunguka kiliporomoka akitazama.
Barabara ya kuelekea Norcia imeharibiwaImage copyright@FRANC_PETRUCCI
Image captionBarabara ya kuelekea Norcia imeharibiwa
Duru zasema kuwa mji wa Amatrice -ambao uliharibiwa na tetemeko la mwezi Agosti, limeharibiwa tena zaidi.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kwamba watu tisa wamejeruhiwa lakini taarifa kuhusu vifo bado hazijatolewa.
Kitovu cha tetemeko hilo lilikuwa kusini mashariki mwa mji wa Perushia.

Mtu aliyevalia kama mti akamatwa Marekani

Tree guyImage copyrightTED VARIPATIS/TWITTER
Mwanamume mmoja nchini Marekani, ambaye ameanza kufahamika kama "binadamu mti", alikamatwa baada yake kuvuka barabara akiwa amevalia kama mti.
Asher Woodworth, kutoka jimbo la Maine nchini Marekani, alijifunika kwa matawi na kuvuka barabara polepole.
Polisi walimsindikiza hadi kando mwa barabara kabla ya kumuweka kizuizini.
Asher baadaye aliachiliwa huru na polisi.
Mwanamume aliyefunikwa kwa matawi
Aliambia BBC kwamba alikuwa akivuka barabara mara ya tatu pale alipokabiliwa na maafisa wa polisi.
Yeye ni mwigizaji mjini Portland, Maine.
Anasema: "Nilipata wazo hili nilipokuwa natafakari sana siku moja."
Anasema alikuwa anataka tu kuwashangaza watu kwa mavazi yake na kuwafanya "watafakari upya kuhusu matarajio yao".
Alikuwa ametumia matawi ya miti ya aina mbalimbali na anasema ilimchukua yeye na rafiki yake saa kadha kukamilisha vazi hilo.
MatawiImage copyrightTOTAL WASTE/TUMBLR
Image captionAlikuwa amepakia picha yenye vazi jingine linalokaribiana na hilo kwenye mtandao wa Tumblr mwezi uliopita
Anasema matawi ya miti aliyokuwa amevalia yalikuwa "yananukia".
Lakini mbona akaamua kuvalia matawi ya miti?
"Huwa nahisi nina uhusiano wa karibu na miti, naipenda sana," aliambia.
Alikuwa pia ametiwa moyo na mpiga picha Charles Freger, aliyepiga picha hii iliyo hapa chini.
Mwanamume aliyefunikwa kwa matawiImage copyrightTOTAL WASTE/TUMBLR
Image captionAsher Woodworth pia aliweka picha hii ukurasa wake wa Tumblr
Baada yake kukamatwa, Asher Woodworth anasema alikaa saa sita kizuizini kabla ya kuachiliwa huru Jumatatu.
Matawi

Rwanda yanunua ndege kubwa ya kisasa zaidi ya Airbus


Shirika la ndege la Rwanda, Rwandair, limezidisha ushindani katika uchukuzi wa ndege Afrika Mashariki na Kati kwa kununua ndege aina ya Airbus A300-200.
Ndege hiyo itawezesha shirika hilo kufika masoko ya Ulaya na bara Asia.
Ndege hiyo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa kimataifa wa Kanombe, Kigali.

Mkuu wa shirika la Rwandair John Mirenge amewaambia waandishi wa habari kuwa ndege hiyo yenye nafasi ya abiria 244 ndiyo ya kwanza katika ukanda huu na ina teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu.

"Ukiwa angani ndani ya ndege hii unaweza kupiga simu, kupata ujumbe wako wa simu, ujumbe wa barua pepe, ujumbe wa WhatsApp na mawasiliano mengine. Haya hayakuwepo katika ndege nyingine tulizo nazo," amesema.
"Hata katika ukanda huu na kwingineko barani afrika hakuna shirika lenye ndege iliyo na uwezo huo."

Ni ndege iliyotengenezwa nchini Ufaransa na kununuliwa kwa kitita cha dolla milioni 200 za marekani.
Safari ya kwanza ya ndege hiyo itakuwa kwenda Dubai

Safari ya kwanza ya ndege hiyo itakuwa kwenda Dubai
Bw Mirenge, anasema safari za shirika la ndege la Rwandair zilikuwa zinajikita sana Afrika magharibi na kati na kwamba ndege hii sasa inakuja kuongeza uwezo wa kuvamia masoko ya Ulaya, Asia na kusini mwa Afrika.
Safari ya kwanza ya ndege hiyo inatarajiwa kufanyika wikendi ijayo tarehe 8 kuelekea mjini Dubai.
Shirika hilo sasa linalenga kusafirisha abiria laki 750 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017.

VIDEO: Aliyekatwa mkono na Baba yake kisa wizi shambani, asimulia ilivyokuwa



Mtu wangu September 30 2016 zimehappen stori nyingi sana nisingependwa upitwe na hii story iliyotokea Kenya, Kituo cha Citizen cha Nchini Kenya kimeripoti kutokea kwa taarifa za Baba mzazi kumkata mtoto wake mikono kutokana na baada ya mtoto huyo kudaiwa  kuiba Mirungi shambani.
Nikawaida yangu kukusogezea story zote ambazo zinatoke kwenye mitandao ya kijamii Tv stations na sehemu mbalimbali na nimekusigezea video ya mkasa huo uliotokea nchini keny unaweza kuitazama hapa chini.
‘Alinitoa hapo kwenye njia na Baba yangu ndio aliyenikata mkono wangu lakini alipokuwa akiondoka watu wengine wakamfuata na kumwambia sijakatika mkono ndio Baba aliporudi nakunimalizia kunikata mkono wangu‘


Tibaijuka agoma kuchukua milioni 200 za tuzo

Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka ametunukiwa tuzo ya heshima ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalfa bin Salman Al Khalifa ikiwa ni utambuzi wa mchango wake wa kuchochea maendeleo
dntibaijuka1110a
Tibaijuka ameyasema jana wakati akizungumza na wanahabari kwa lengo la kuelezea namna alivyopatiwa tuzo hiyo pamoja na fedha kiasi cha dola laki moja ambayo amekataa kuichukua kutokana na hofu ya kukumbwa na kashfa kama ile iliyomkumba wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali ya awamu ya nne.
Pia alisema kuwa tuzo hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Bahrain na hutolewa baada ya miaka miwili kwa mtu ambaye ametoa mchango mkubwa katika kutatua changamoto za sekta mbalimbali za kiuchumi ambazo zinawakumba wananchi.
Profesa Tibaijuka alifafanua kuwa tuzo hiyo imetokana na kushughulikia malengo ya milenia wakati akiwa anafanya kazi katika Umoja wa Mataifa (UN) na kusema kuwa tuzo hiyo ni heshima kwa watanzania kwani alienda kuwawakilisha kwenye umoja huo.

Rais wa Botswana amtaka Robert Mugabe kujiuzulu

Rais wa Botswana Ian Khama amemtaka Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kujiuzulu mara moja kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
_91331430_iankhama

Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe
Ameambia Reuters kuwa taifa la Zimbabwe linahitaji uongozi mpya ili kukabiliana na changaomoto za kisiasa na za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.
“Ni wazi kwamba umri wake na hali ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa kutoa uongozi ambao unaweza kulinusuru taifa hilo,”.
Bwana Mugabe ameliongoza taifa hilo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Bwana Khama amemlaumu kiongozi huyo kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.
Amesema mgogoro uliopo Zimbabwe umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku wengine wakielekea Botswana ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa Zimbabwe.
Khama anasema kuwa ataondoka afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ,huku akiwashtumu viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda mrefu.

Wafanyakazi nane wafukuzwa kazi kisa unene

Habari hii imeripotiwa na BBC ambapo imetokea nchini Misri kwenye television ya Taifa hilo ambapo imewafukuza kazi wafanyakazi 8 wa kike na kuwashauri waende wakapunguze uzito wa mwili.
Chama cha Radio na Televisheni nchini Misri ( ERTU) kimewapa wanawake hao muda wa mwezi mmoja kupunguza uzito kabla ya kuruhusiwa kuonekana tena kwenye television.
BBC
Tangazo hilo limezua lawama kutoka kwa watangazaji walioathiriwa ambapo mmoja wao Khadija Khattab, mtangazaji wa kituo cha Channel 2, amesema kuwa anataka watu ndio watazame kipindi chake na waamue wenyewe ikiwa ana uzito wa juu.

Picha: Tazama uzinduzi wa mashindano ya Olimpiki 2016 Brazil

Mashindano ya Olimpiki 2016 Ijumaa hii yalizinduliwa rasmi mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil na kupambwa na burudani ya tamaduni za nchi hiyo.
36EB96AF00000578-3726239-image-a-193_1470444704006
Pamoja na hivyo ufunguzi wa mashindano hao haukubarikiwa na raia wengi wa Brazil waliojikusanya nje ya uwanja kuandamana kuyapinga.
Wananchi hao walipambana na polisi waliotumia mabomu ya machozi kuwatawanyisha. Ndani ya uwanja huo wa Maracana wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000 kulikuwa na viti vitupu kibao. Tazama picha mbalimbali za ufunguzi huo.

36EA4EE500000578-3726239-image-a-26_1470437762551

36EB6E2100000578-3726239-image-a-133_1470441937041

36EB9D0300000578-3726239-image-a-217_1470445477840

36EBA62000000578-3726239-image-a-247_1470447087755

36EBBCCA00000578-3726239-image-a-280_1470449502306

36EBEBE800000578-3726239-image-a-39_1470459539188

36EC2DB400000578-3726239-image-a-294_1470450133016

36EC4A7900000578-3726239-image-a-30_1470456617317

36EC6BBA00000578-3726239-image-a-364_1470455162765

36EC7A5B00000578-3726239-image-a-352_1470455071137

36EC7E9F00000578-3726239-image-a-354_1470455073743

36EC16CD00000578-3726239-image-a-270_1470448870038

36EC71CD00000578-3726239-image-a-359_1470455095301

36EC147D00000578-3726239-image-a-267_1470448859222

36EC286A00000578-3726239-image-a-286_1470449963479

36EC596D00000578-3726239-image-a-346_1470454919880

36EC355000000578-3726239-image-a-3_1470455993609

36EC567500000578-3726239-image-a-337_1470453823628

36EC574900000578-3726239-image-a-351_1470455061750
36ECE7D900000578-3726239-image-a-15_1470472498894

Video: Britney Spears ft. G-Eazy – Make Me

Britney Spears is looking for a leading man to cast in her new video for “Make Me…” featuring G-Eazy.

Tazama Utajiri wa Mwanasiasa mtata wa Marekani Donald Trump


Najua kuna watu wangu mnafuatilia mchakato wa uteuzi wa kumpata mgombea urais Marekani. Dolnad Trump ni moja ya wagombea wa Republican ambao wamechukua headline sana na anaonekana kama kuelekea kufanikiwa hivi, usishangae ikaishie anaingia white house.
Mwanasiasa huyu mtata amezaliwa sehemu ambayo wazazi wana pesa, lakini mali zake zimekuwa zikiongezeka kutokana na biashara zake, sasa ana miaka 69 na ana utajiri wa unaokadiriwa kufika  Dola bilioni 8.7 kwa takwimu za june 2015. Donald Trump alianza kufanya kazi kwenye kampuni ya baba yake na akanza kupiga mpaka deal kubwa ukitaka kuufahamu zaidi utajiri wa mwanasiasa huyu na billionare angalia picha hizi hapa chini.
1
Enzi za ujana wake Donald 
2
Akionekana na helkopita yake mwenyewe
3
Hii ni moja ya Uwanja wake wa Gofu uliopo Washington DC
5
Ndege yake aina ya Boeing 727-23
6
muonekano wa ndege kwa ndani
7
.
8
.
9
.
10
.
11
Donald Trump na Mkewe Melania Knauss Trump
12
Mjengo wa Donald Trump
13
Muonekano wa Ndani wa mjengo wa Trump
14
.
15
Hili ni eneo lake jingine la kuishi, Palm beach Florida
16
Hili ni eneo la Swimming pool kwenye nymba yake ya kuishi
17
hapa ni nyumba ya zamani ya Trump
18
Huu ni mwonekano wa ndani wa nymba ya Trump ya zamani
19
Ukumbi wa Cinema kwenye mjengo huo 
20
Unaweza ukaangalia moja muonekano wa Dining room kwenye mjengo wake huo wa zamani
24
25
.