Mashindano ya Olimpiki 2016 Ijumaa hii yalizinduliwa rasmi mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil na kupambwa na burudani ya tamaduni za nchi hiyo.
Pamoja na hivyo ufunguzi wa mashindano hao haukubarikiwa na raia wengi wa Brazil waliojikusanya nje ya uwanja kuandamana kuyapinga.
Wananchi hao walipambana na polisi waliotumia mabomu ya machozi kuwatawanyisha. Ndani ya uwanja huo wa Maracana wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000 kulikuwa na viti vitupu kibao. Tazama picha mbalimbali za ufunguzi huo.
0 comments:
Post a Comment