Wanafunzi wa kiume 11 wa shule za msingi Sombetini jijini Arusha wametuhumiwa kufanya ngono na mbwa eneo la mto Ngarenaro. Watoto hao ni wa miaka kati ya miaka saba na 11 wa darasa la tatu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha , Charles Mkumbo amesema jeshi la polisi haliwezi kuwafungulia kesi wanafunzi hao ambao wamekiri kufanya vitendo hivyo mara kadhaa, kutokana na umri wao kuwa mdogo. Kamanda Mkumbo amesema………..
>>>’Kisheria, ili mtu aweze kushitakiwa na hilo kosa anapaswa angalau mtu mzima kuanzia miaka 13 na kuendelea, mtoto wa miaka 10 na kurudi nyuma kisheria hastahili kushtakiwa kwa jambo lolote alilolitenda la kijinai, mtoto miaka 11, 12 lazima ujilidhishe kwamba wakati anafanya kosa alikuwa na uelewa wa kutosha kwamba kosa hilo analolitenda ni kosa’
Aidha amesema jeshi hilo linawatafuta vijana waliowafundisha kufanya mapenzi na mbwa wakati watoto hao wakiendelea kupata ushauri wa kitaalam
0 comments:
Post a Comment