Latest News
Loading...

Bifu: Filamu aliyocheza Fid Q ambayo hataki uione

Kabla ya kupata tobo na kuwa mmoja wa wana hip hop wanaoheshimika zaidi Tanzania, Fid Q aliwahi kufanya mishe mishe mingi ikiwemo kuwa muigizaji wa ‘bongo movie.’
14052710_285256755189367_1903409507_n
Yeye na Sugu waliigiza filamu ya maisha ya muziki iitwayo Bifu. Kutokana na kuwa na kiwango cha chini, Fid Q hataki uione filamu hiyo kwakuwa anahisi kwa alipofika inamtoa nishai!
“Kiukweli ROHO IMENIUMA sana kukuta YouTube bado hawajaitoa hii trela,” Fid alimjibu mpiga picha maarufu MX Carter aliyeweka link ya trailer yake kwenye Twitter.
“Daah!halafu Jana nimekutana na moja wa directors halafu akanipa business card yake ili ni mtafute..mimi?,” ameongeza.
“Ile subtitle ndo nilikua sitaki kabisa muistukie.. Ni ukweli TULIKOTOKA NI MBALI.. lakini wengine TUMETOKEA MBALI ZAIDI. Kinachoniuma zaidi waigizaji wote hatukupata access ya kuingia editing room.Tulikutana na filamu yetu mtaani.”
Filamu ya Tanzania ya maisha ya muziki iliyowahi kufanya vizuri zaidi ni Girlfriend ambayo iliwahusisha wasanii kama TID, Monalisa, AY, Saida Simba Kilumanga na wengine.

0 comments:

Post a Comment