Latest News
Loading...

Hatimaye Msanii Ney wa mitego kasalimu amri

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego ameanza kutekeleza baadhi ya maagizo aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa baada ya kufungiwa kwa wimbo wake wa ‘Pale Kati’.
Rapper huyo alipewa adhabu hiyo pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni 1 baada ya kukutwa na makosa matatu likiwena la kutojisajiri katika baraza hilo.
Katika taarifa aliyotoa Nay wa Mitego, ameonyesha kujuta huku akiwaomba radhi mashabiki wa muziki wake kama ambavyo aliagizwa na BASATA.
“Wakati naandika wimbo “Pale Kati” nilikua nimeangalia nyimbo zilizowahi kutoka nyuma na zilizoko sokoni sasa, sikuona kama mistari yake ina matatizo. Lakini baada ya kukaa pamoja na kusikiliza mstari kwa mstari tumegundua kwamba kuna baadhi ya mistari ilikua ina maneno makali. Hivyo basi naomba radhi kwa mtu yeyote alieumizwa au kukwaza na mistari hiyo. Tusikilizie kifuatacho.!! “Pale kati” jamani,” aliandika Nay wa Mitego kupitia instagram yake.
Pia rapper huyo ametakiwa kujisajiri katika baraza hilo pamoja na kuachana na kuimba vyimbo ambazo zinawazalilisha akina dada.

0 comments:

Post a Comment