Ikiwa ni siku ya mwisho ya dirisha la usajili nchini Uingereza klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa kiungo wa kati Alex Oxlade-Chamberlain kutoka katika klabu ya Arsenal kwa kiasi cha pauni milioni 35.
Chamberlain mwenye umri wa miaka 24 awali alikuwa akiwindwa na mabigwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza Chelsea lakini alikataa uhamisho huo siku ya Jumanne na sasa amejiunga na Liverpool kwa mkataba wa miaka mitano ambapo atakuwa akipokea £120,000 kwa wiki.
Kiungo huyo wa kati ameichezea klabu ya Arsenal mara 198 tangu ajiunge nayo kutoka katika klabu ya Southampton mnamo mwezi Agosti mwaka 2011 na amefanikiwa kuifungia timu hiyo jumla ya mabao 20.
Diego Costa kusajiliwa kwa mkopo HispaniaXhaka, Mustafi, Perez na Calum Chambers wataikacha Arsenal?Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa anafurahi kumsajili mchezaji huyo mwenye uwezo mkubwa. Kocha hoyo ameongeza kuwa Chamberlain hakufanya maamuzi mepesi kuhama kutoka katika klabu kubwa lakini pia amefanya maamuzi maamuzi mazuri kwani amejiunga na klabu kubwa pia yenye vijana wenye vipaji.
Oxlade-Chamberlain akisaini mkataba
Tayari klabu ya Liverpool imemsajili winga Mohammed Salah kutoka Roma kwa pauni milioni 34, beki Andrew Robertson kutoka Hull City kwa pauni milioni 8 na mshambuliaji Dominic Solanke.
Latest News
Loading...
Liverpool yakamilisha usajili wa Chamberlain
Related Posts:
Maroune Fellain: Wachezaji Manchester United tunatakiwa kuwajibika Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Maroune Fellain amekiri kuwa wapo katika wakati mgumu baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo. Fellain amefunguka kuwa yeye na wachezaji wenzake wanatakiwa kuwajibika katika hali… Read More
Valencia CF wamtimua kocha wao Pako Ayesteran Klabu ya Valencia CF imetangaza kumfukuza kazi meneja Pako Ayesteran kufuatia kufanya vibaya kwa kikosi hicho kuwa na mwenendo mbaya tangu walipoanza msimu wa 2016/17. Valencia CF wamemfukuza Ayesteran baada ya miezi sit… Read More
VIDEO: Magoli ya mechi ya Simba vs Majimaji Septemba 24, Full Time 4-0 Jumamosi ya Septemba 24 2016 wekundu wa Msimbazi Simba ambao wanaelekea kucheza mchezo wao na watani zao wa jadi Yanga, walicheza mchezo wao wa sita wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Majim… Read More
VIDEO: Baada ya mechi 9 dhidi ya Chelsea, Arsenal ndio kapata ushindi wa kwanza Usiku wa Septemba 24 2016 jiji la London lilikuwa busy kwa upande wa mashabiki wa soka kwani mashabiki wa timu kubwa za Arsenal na Chelsea walikuwa busy kufuatilia mchezo dhidi ya vilabu vyao ambavyo vyote vinatokea nd… Read More
Mwanasoka wa Sierra Leone afariki katika ajali mbaya ya gari Aliyekuwa mwanasoka wa kimataifa, raia wa Sierra Leone, Mamadu Alphajor Bah amefariki dunia katika ajali mbaya ya barabarani iliyofanyika karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Freetown. Mamadu Alphajor Bah aliwahikucheza soka ya … Read More
0 comments:
Post a Comment