Latest News
Loading...
Home »
KITAIFA
» "Sethi Amewekwa Puto Tumboni" Kutokana na Matatizo ya Kiafya upande wa Utetezi Umeeleza
"Sethi Amewekwa Puto Tumboni" Kutokana na Matatizo ya Kiafya upande wa Utetezi Umeeleza
Upande wa utetezi umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi amewekewa ‘Puto’ tumboni kutokana na ugonjwa unaomkabili hivyo asipohudumiwa inavyotakiwa anaweza kupoteza maisha.
Mbali ya Seth, mwingine ni Mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya TSh 309,461,300,158.
Wakili wa utetezi, Joseph Mwakandege amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mteja wake Seth anatakiwa apelekwe Hospital ya Taifa Muhimbili lakini hadi sasa hajapelekwa na ni dhahiri upande wa mashtaka umedharau amri mbili za Mahakama.
”Ugonjwa uliosababisha Seth atakiwe kwenda Muhimbili ni baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa ambapo tumboni kwake kumewekwa Balloon ‘Puto’ hivyo asipohudumiwa ipasavyo inaweza kusababisha kifo, naomba mshtakiwa apelekwe Muhimbili kwa sababu ni Hospitali ya juu na yenye vifaa na watalaamu wa kutosha“
Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali Vitalis Peter amedai kuwa Magereza hawapangiwi wampeleke wapi mshtakiwa ambaye ni mgonjwa bali wana utaratibu, Hospitali na watalaam wao.
”Mshtakiwa alianza kupelekwa Hospital ya Magereza, kisha Hospital ya Amana ambapo alikutana na daktari mtalaam kutoka Muhimbili na aliweza kumuangalia afya yake, hivyo hoja ya kwamba hatujatekeleza amri ya Mahakama sio kweli.”
Baada ya kusema hayo, Hakimu Shahidi amesema alishatoa amri mara mbili kwamba Seth akatibiwe Muhimbili na kusisitiza akatibiwe >>>”Nasisitiza tena, mshtakiwa akatibiwe Muhimbili, sioni kama kuna sababu ya kulumbana, kesi imeahirishwa hadi September 14, 2017.”
Related Posts:
Mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi na Jeshi la polisi Kuwekwa hadharani leo Mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises uliosababisha kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya fedha katika Jeshi la Polisi, leo unatarajiwa kuwasilishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). M… Read More
Acacia kuilipa Serikali Dola mil.20 KAMPUNI ya Acacia Mining PLC imesema itailipa serikali kodi ya dola za Kimarekani milioni 20 mwaka huu baada ya kusainiwa mkataba wa maridhiano kati yake na Mamlaka ya Mapato (TRA) mwezi uliopita jijini Dar es Sa… Read More
Wachina kizimbani kwa kukwepa kulipa kodi Raia wawili wa China, Ma Jun na Huifang Ma leo wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili likiwamo la kushindwa kutumia Mashine ya Kodi za Kielektroniki (EFDs) katika biashara zao.Jun na Ma,… Read More
Maalim Seif Sharrif Hamad Kutoa Mwelekeo Wake Kisiasa Kesho Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu. M… Read More
Msanii wa Muziki wa dansi Ndanda Kosovo Afariki Dunia Msanii wa muziki wa dansi Ndanda Kosovo amefariki dunia asubuhi ya leo katika hosptali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanamuziki mwenzake Kardinal Gento, Ndand… Read More
0 comments:
Post a Comment