Latest News
Loading...

Makongoro Nyerere Awataka Watanzania Kuchangamkia Fursa Zilizopo Afrika Mashariki


Wananchi wa Tanzania wametakiwa kuchangamkia nafasi za kufanya baishara zilizopo kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana na kuwepo makubaliano ambayo yanawapa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kufanya biashara kwa uhuru.

Hayo yalisemwa jana na Mbuge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere ambaye alidai kuwa nchi za Afrika Mashariki zinashirikiana kwa mambo mbalimbali ikiwepo umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na shirikisho wa kisiasa.

Alisema kupitia makubaliano hayo Watanzania wana nafasi ya kwenda kufanya baishara katika nchi zingine bila kuzuiliwa na hivyo kuwa na nafasi ya kusambaza bishaa zao katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Huu ni muda wa Watanzania kuchangamkia nafasi zilizopo za kufanya baishara kwa nchi za Afrika Mashariki, vikwazo zilivyopo kwa sasa ni wananchi wengi wa Afrika Mashariki bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu hilo lakini tumejipanga katika hilo,” alisema Nyerere.

Alisema kwa kutambua changamoto hiyo ya wananchi wengi kutokufahamu nafasi hiyo, wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania wataendesha programu ya kuwaelimisha Watanzania jinsi wanavyoweza kunufaika na ushirikiano huo.

Alisema programu hiyo ilianza Aprili 4 na itafanyika hadi Aprili, 23 ambapo kwa kuanza wamepanga kukutana na Kamati za Bunge, Taasisi za Elimu ya Juu, vyombo vya habari, kutembelea soko la Kariakoo na soko la Samaki la Feri.

Pia Nyerere aliwataka Watanzania kuwa na mazoea ya kutafuta taarifa mbalimbali kupitia mitandao kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kukutana na fursa nyingi ambazo hawakuwa wakizifahamu awali.

0 comments:

Post a Comment