MOROGORO: Ikiwa takriban siku 40 tangu baba yao, Dk. Ephraim Njawala Mwampamba, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) afariki dunia, mwanaye Mwisho Ephraim Mwampamba ameburuzwa mahakamani na kaka yake, Robert Ephraim Mwampamba, Jumatatu iliyopita.
Kesi hiyo namba 197/2016 ilisikilizwa katika Mahakama ya Mwanzo Chamwino iliyopo Mazimbu mkoani hapa, ambapo Robert alimburuza mahakamani hapo mdogo wake huyo waliyechangia baba, akimtuhumu kumtukana matusi ya nguoni huku sehemu kubwa ya matusi hayo yakiwa ya kibaguzi.
Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Mwisho alitokea mahabusu alikolala kwa siku moja ambapo baada ya kesi kusikilizwa, alipata dhamana huku ikidaiwa kuwa kesi hiyo imemkalia vibaya kutokana na ushahidi unadaiwa upo.
Akisoma kesi hiyo mahakamani hapo, Hakimu Amina Chungulu alidai Mwisho anatuhumiwa kumtukana matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini) kupitia namba za simu (tunazihifadhi) ambayo inaaminika inamilikiwa na Mwisho Mwampamba.
Mwisho alipoulizwa na hakimu huyo alikana kutenda kosa hilo na Robert alipoulizwa kama ana ushahidi ndipo aliposema anao wa meseji hizo kwenye simu yake.
Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 11, mwaka huu huku Robert akitakiwa kufika mahakamani hapo na meseji hizo kama ushahidi.
Aidha, Hakimu Amina alisema dhamana iko wazi kwa mshitakiwa; mdhamini mmoja na shilingi laki 4 ambapo kaka mwingine wa Mwisho aliyezaliwa naye baba mmoja na mama mmoja, lsambe alimdhamini mdogo wake huyo.
Latest News
Loading...
Mwisho Mwampamba Kortini..Alala Mahabusu Siku Mbili Kisa Matusi ya Nguoni...
Related Posts:
Wabunge Wataka TANESCO Itumbuliwe Majipu Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara wamemtaka Rais John Pombe Magufuli kulitumbua jipu shirika la umeme Tanesco kwa kununua transfoma kutoka nje ya nchi licha ya … Read More
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella aamuru kurudiwa kwa uhakiki wa watumishi HEWA mkoa wa Mwanza Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameagiza kurudiwa upya kwa zoezi la uhakiki la kuabaini watumishi hewa katika mkoa wa Mwanza, ikiwa ni mpango wa kubaini wale wote wanao lipwa mishahara bila kufanya kazi, zoezi hil… Read More
Wanajeshi wa Tanzania Waingia katika kashfa ya ngono DRC Ujumbe wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (Monusco) umeanzisha uchunguzi dhidi ya wanajeshi wa Tanzania wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya udhalilishaji kingono. … Read More
Rais wa Zanzibar Dkt. Shein amteua Hamadi Rashid kuwa mjumbe wa Baraza la wawakilishi Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua mwenyekiti wa chama cha ADC Hamad Rashid Mohamed kuwa mjumbe wa Baraza la wawakilishi. Uteuzi huo wa Rais Dkt Shein umefuata baada ya leo kutoa… Read More
Walimu Walazwa UCHI na Kuchapwa Viboko Ofisi ya Elimu wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani imelazimika kuwapa likizo walimu saba wa Shule ya Msingi Mingwata ili kuwajenga kisaikolojia baada ya kukithiri kwa matukio ya kishirikina yanayowakumba katika shule hiyo.… Read More
0 comments:
Post a Comment