Diamond Platnumz anachekelea tu sasa hivi kwasababu wimbo wake Kidogo aliowashirikisha mapacha wa P-Square umepanda daraja zaidi kwenye playlist za redio yenye heshima kubwa Uingereza, BBC Radio 1Xtra.
Na ili kujua ukubwa wa hiki kilichotokea ni vyema ukafahamu kuwa ni nyimbo chache sana za Afrika zilizowahi kuingia kwenye playlist ya kituo hicho maarufu kwa burudani UK.
Tuliripoti siku chache zilizopita kuwa wimbo wake huo umeingia rasmi kwenye playlist zake lakini ukawa umewekwa kwenye orodha C. Na sasa wimbo huo umepanda hadi orodha B.
Diamond hajaficha furaha yake kufuatia kupanda daraja kwa wimbo wake huo.
“Dear God i wanna thank you, for everything …. #KIDOGO on the BBC Radio 1xtra PlayList from C list last week to B list this week…. thanks alot BBC Radio 1xtra and my all UK fans for the Big Support,” ameandika kwenye Instagram.
Iwapo wimbo huo utapanda hadi orodha A, maanake ni kuwa utakuwa kwenye rotation kubwa zaidi kwa siku huku pia akipokea mrabaha mkubwa kutokana na kuchezwa ngoma yake – wenzetu hawachezi ngoma za wasanii bure etii!
0 comments:
Post a Comment