Ikiwa ni siku kadhaa tangu tamko la msajili wa vyama vya siasa kueleza msimamo na ushauri kuhusu mgogoro unaoendelea kwenye chama cha wananchi CUF, katika msimami uliotolewa na msajili wa vyama ulieleza kuwa Profesa Ibrahim Lipumba ni mwenyekiti halali wa CUF vilevile wanachama waliokuwa wamefukuzwa na kusimamishwa ni wanachama halali
Baada ya tamko hilo Profesa Ibrahim Lipumba alifika katika ofisi za chama CUF makao makuu jijini Dar es salaam akisindikizwa na wafuasi wake kwa ajili ya kuanza rasmi shughuli za uenyekiti wa chama.
Leo September 26, 2016 taarifa iliyotolewa na kituo cha ITV imeeleza kuwa Baraza kuu la uongozi Taifa wa Chama cha Wananchi CUF limefanya kikao cha kujadili suala hilo na maamuzi yaliyotolewa na baraza hilo ni kumfukuza uanachama Profesa Ibrahim Lipumba kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kutumia vijana kuvunja ofisi za CUF na kuingia kwenye ofisi hizo.
0 comments:
Post a Comment