Latest News
Loading...
Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Prof. Lipumba basi tena CUF, hii ndiyo hatua iliyochukuliwa na baraza kuu la uongozi CUF

Ikiwa ni siku kadhaa tangu tamko la msajili wa vyama vya siasa kueleza msimamo na ushauri kuhusu mgogoro unaoendelea kwenye chama cha wananchi CUF, katika msimami uliotolewa na msajili wa vyama ulieleza kuwa Profesa Ibrahim Lipumba ni mwenyekiti halali wa CUF vilevile wanachama waliokuwa wamefukuzwa na kusimamishwa ni wanachama halali
Baada ya tamko hilo Profesa Ibrahim Lipumba alifika katika ofisi za chama CUF makao makuu jijini Dar es salaam akisindikizwa na wafuasi wake kwa ajili ya kuanza rasmi shughuli za uenyekiti wa chama.
Leo September 26, 2016 taarifa iliyotolewa na kituo cha ITV imeeleza kuwa Baraza kuu la uongozi Taifa wa Chama cha Wananchi CUF limefanya kikao cha kujadili suala hilo na maamuzi yaliyotolewa na baraza hilo ni kumfukuza uanachama Profesa Ibrahim Lipumba kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kutumia vijana kuvunja ofisi za CUF na kuingia kwenye ofisi hizo.



Kesi imemgeukia Lyatonga Mrema, anatakiwa kulipa MILIONI 40 kabla ya tarehe 5 June

Kesi ya Lyatonga Mrema kupinga ushindi wa Ubunge wa James Mbatia jimbo la Vunjo ilikua Mahakamani tena April 4 2016 ambapo jipya lililotangazwa ni kwamba Mahakama kuu kanda ya Moshi imeridhia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia na Agustino Mrema kwa shauri hilo kuisha na kwamba Mbatia ndiye Mbunge halali wa Vunjo na Mrema atatakiwa kulipa sehemu ya gharama za mawakili wa Mbatia shilingi Milioni 40.
Unaweza kumsikiliza James Mbatia hapa chini akichanganua ishu ya hizo Milioni 40 japo yeye amemsamehe Mrema.