Latest News
Loading...

VIDEO: Gari lililozama Baharini Kivukoni Dar es salam April 20 2016

April 20 2016 gari aina ya Toyota Hiace lililokuwa ndani ya Pantoni kuelekea Kigamboni Dar es salaam liliserereka na kuzama baharini ambapo inasadikiwa lilikuwa na watu wawili, uokoaji ulifanyika ambapo asubuhi jeshi la zimamoto na uokoaji lilifanikiwa kuupata mwili mmoja na mchana mwili wa pili wa Nice Karago ukapatikana...

Source:AyoTV

Nyota ya Mbwana Samata Yazidi Kung'aa Baada ya Ushindi Mwingine Mnono wa Timu yake...

Usiku wa April 20 2016 kocha wa KRC Genk Peter Maes kaendelea kumuamini na kumpa nafasi ya kuanza katika first eleven yake nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayeichezea klabu hiyo Mbwana Samatta, Maes amempa nafasi Samatta ya kuanza mchezo wa pili mfululizo.

Licha ya kuwa KRC Genk walikuwa nyumbani katika uwanja wao wa Cristal Arena kukabiliana na vinara wa Ligi hiyo Club Brugge, Maes kamuamini Samatta na kumpa nafasi katika mchezo huo mgumu ulio malizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 4-2. Samatta amecheza kwa dakika 75 na dakika ya 76 alitoka akaingia Nikolaos Karelis.

Samatta anakuwa amefikisha jumla ya mechi tatu alizoanza akiwa na KRC Genk katika mechi hizo amefunga mechi mbili goli moja moja katika kila mchezo, magoli ya KRC Genk ya leo yamefungwa na Onyinye Ndindi dakika ya 15, Alejandro Melero dakika ya 42, Thomas Buffel dakika ya 45 na Jeren Uronen dakika ya 73.

Kwa Sasa Genk Inashikilia Nafasi ya Nne Katika Ligi hiyo

TUCTA Yapinga Mpango wa Rais Magufuli Kukata Mishahara ya Watumishi wa Umma Kutoka Milioni 40 hadi 15 Kwa Mwezi

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta) limepinga mpango wa Rais John Magufuli wa kukata malipo ya mishahara ya watumishi wa umma kutoka Sh40 milioni kwa mwezi hadi Sh15 milioni.

Akizungumza na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Kanda ya Ziwa jijini Mwanza jana, Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Hezron Kaaya alisema uamuzi huo ni kinyume na sheria na utaligharimu Taifa iwapo wahusika wataamua kwenda mahakamani kupinga mishahara yao kupunguzwa. 

“Watendaji hawa hawakujipangia mishahara wao wenyewe, bali malipo haya yalipangwa na bodi za mashirika na taasisi husika ambazo kisheria zimepewa mamlaka hayo. Malipo haya hayawezi kupunguzwa kwa kauli za kisiasa bila kuzingatia mahitaji ya kisheria,” alisema.

“Iwapo Serikali itatekeleza lengo hili bila kuwapo mjadala mpana na makubaliano ya kisheria kati ya wahusika, basi ijiandae kulipa mamilioni ya fedha kama fidia iwapo watakaokatwa mishahara yao watakwenda mahakamani.”

Akiwa mjini Chato wakati wa mapumziko ya wiki moja, Rais Magufuli alitangaza kupunguza mishahara ya juu kutoka Sh40 milioni hadi Sh15 milioni kwa mwezi, akisema wapo watumishi wa umma wanalipwa masilahi manono na kuishi kama wako peponi, huku wanaolipwa Sh300,000 wakiishi kama wako jehanamu.

Kaaya aliishauri Serikali kuendelea kuwalipa mishahara hiyo minono wahusika hadi mwisho wa mikataba yao, ndipo lengo la kuipunguza litekelezwe ama kwa kuwapa wahusika mikataba mipya au kuajiri watu wengine.

“Serikali inaweza kuwa na nia njema kupunguza tofauti kubwa ya mishahara kati ya kada ya juu na chini, lakini utekelezaji wake lazima usubiri muda mwafaka mikataba ya sasa itakapomalizika,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine; Tucta imepinga hatua zinazochukuliwa na baadhi ya mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya ya kutangaza kuwasimamisha kazi watumishi wa umma ambao hawapo chini ya mamlaka zao kinidhamu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla Aonja Moto wa UKAWA.....Madiwani 34 Wakiongozwa na Meya wao Wasusia Kikao chake cha Kujitambulisha


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amekumbana na joto la Mbeya baada ya meya wa jiji hilo, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani wake 34 kususia kikao chake cha kujitambulisha kwa wananchi, baada ya kudaiwa kwenda kukagua Soko la Mwanjelwa bila kumpa taarifa yoyote meya wa jiji hilo.

Meya alifikia uamuzi huo ndani ya ukumbi wa Mkapa muda mfupi kabla ya Makalla kuanza kuzungumza na watumishi wa jiji, wananchi, wazee maarufu, viongozi wa dini na machifu ambapo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Sabi alimkaribisha Meya Mwashilindi kuzungumza chochote kwa niaba ya madiwani wake.

Hata hivyo, Meya Mwashilindi alipochukua kipaza sauti alisema: “Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, nakumbuka kwa mara ya kwanza kukutana na wewe tulizungumza kwamba tufanye kazi, siasa zimekwisha. Lakini masikitiko yangu ni kwamba leo hii umekwenda Soko la Mwanjelwa bila ya mimi mwenye jiji kupewa taarifa yoyote wala madiwani wangu. Sasa hiki kikao hakinihusu hivyo muendelee na kikao chenu.”

Baada ya kusema maneno hayo alikabidhi kipaza sauti kwa mkuu wa wilaya, kisha akachukua nyaraka zake akainuka pamoja na madiwani wote kupitia Chadema na kutoka ukumbini huku wakisikika wakisema,‘hizi ni siasa ambazo tulizikataa, lakini wanatulazimisha kuendesha siasa. Hatuwezi kupuuzwa kwa kiasi hiki.”

Mkuu wa Wilaya, Mnasa alisema anaamini taratibu na ratiba yote ilipangwa vizuri hivyo hawaoni sababu ya madai ya madiwani hao kwamba hawakushirikishwa kwenye ziara hiyo, wao kama wawakilishi wa Rais hawaangalii siasa, bali wanaangalia uchapakazi na siyo masuala ya siasa.

Akizungumzia kitendo cha meya na madiwani wake kususia kikao hicho, Makalla alisema ‘Nashangazwa na uamuzi wa madiwani hawa kwa kitendo hiki, kwani siku ile nilipotembelea Shule ya Sekondari Iyunga, nilisema kwamba Aprili 20 ambayo ndiyo leo (jana) nitakuwa na ziara ya jiji na kabla ya kikao nitataka kutembelea Soko la Mwanjelwa,” alisema Makalla.

Alisema suala la meya na madiwani wake kutoshirikishwa kwenye ziara ya kwenda Soko la Mwanjelwa halimhusu, kwani mwenye wajibu wa kupeana taarifa ni kwenye ngazi ya halmashauri ya jiji, lakini siyo yeye (Makalla).

“Jamani mimi sijaja kufanya siasa nimekuja kufanya kazi ya wananchi na nilishatahadharisha jambo hili, sasa kwa kitendo hiki ndiyo siasa na wananilazimisha kufanya siasa, lakini wao ndiyo watahukumiwa na wananchi. Na ninasema kama Mola ataendelea kunilinda kubaki katika mkoa mwaka 2020 nitakwenda kuwaambia hiki kinachofanyika sasa na wawakilishi wao,” alisema Makalla.

Awali Makalla akiwa katika Soko la Mwanjelwa alinusa harufu ya ufisadi kwenye soko hilo na kuagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa huo, kufanya uchunguzi ndani ya wiki nne wa uhalali wa fedha kiasi cha Sh22.9 bilioni iliyotumika katika ujenzi huo ukiwa ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.

Makalla alitoa agizo hilo jana mchana baada ya kutembelea soko hilo na kuzungumza na wafanyabiashara wa jijini hapa, ambao walimueleza wanashindwa kumudu gharama ya upangaji ya vyumba vya biashara ambayo inaanzia kiasi cha Sh500,000 kwa chumba kimoja kwa mwezi, ndiyo maana hawataki kuingia ndani ya soko hilo.

Mwenyekiti wa soko hilo, Peter Chacha alimueleza Makalla kwamba wasipokuwa makini soko hilo litabaki gofu, kwani wafanyabiashara hawataki kuingia kwa kuogopa gharama kubwa ya vyumba hivyo, alimuomba afanye awezalo kukaa chini na uongozi wa benki ambao unadai fedha zao kwa jiji na kuona namna ya kupunguziwa gharama hiyo.

“Ni kweli wenzetu jiji, wametingwa na deni la mkopo kutoka Benki ya CRDB, ndiyo maana wamekuja kutubana sisi wafanyabiashara kwa kutupangia chumba kuanzia Sh500, 000 hadi Sh 800,000, kitu ambacho hatuwezi kumudu hata kidogo,”alisema Chacha 

Baada ya kusikiliza kilio cha wafanyabiashara hao, Makalla alisema kiasi cha Sh22.9 bilioni iliyotumika kwenye ujenzi wa soko hilo haiendani na thamani yake, hivyo vyombo vya dola vikiongozwa na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mbeya, wanafanya uchunguzi wa kina na kuwanasaka wale wote waliohusika kwenye mchakato mzima wa ujenzi wa soko hilo.

“Nataka kupata taarifa ya mchanganuo mzima wa namna ya fedha ilivyokopwa, ilivyotumika na mkataba wake ulivyokuwa ndani ya wiki nne, taarifa hii niipokee na wale watakaobainisha kufuja fedha watapelekwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

"Kwenye hili, kuna watu waliotufikisha hapa, Sh22.9 bilioni iliyotumika kwenye ujenzi huu haiendani na ujenzi wa soko hili, kuanzia muda uliotumika na gharama ya kodi ya upangishaji wa vyumba siyo rafiki ni kubwa mno, hivyo jiji na CRDB mkae muone namna ya kupunguza gharama hiyo, kwani hali ilivyo sasa lile soko litabaki gofu."

Mazito yazidi fichuka dhidi ya Anne Kilango, Baada ya Idadi ya Watumishi Hewa Shinyanga Kuongezeka Hadi 226

Rais John Magufuli ameendelea kumng’ang’ania aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango baada ya kusema idadi ya watumishi hewa katika mkoa huo imeongezeka kutoka 45 hadi 226.

Aprili 11, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Kilango kwa kosa la kutangaza kuwa mkoa huo hauna watumishi hewa, lakini ikabainika baada ya Ikulu kufanya uchunguzi wake kuwa kulikuwa na watumishi hewa 45.

Akizungumza juzi wakati wa uzinduzi wa Daraja la Nyerere Kigamboni, Rais Magufuli alisema amekuwa habahatishi kila anapokuwa akichukua uamuzi wa kutumbua jipu.

Alitoa kauli hiyo dakika chache baada kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe na kusema hatakuwa na mzaha katika utumbuaji wa jipu.

Alisema Watanzania wameteseka sana hivyo wanatakiwa kutumikiwa.

Huku akishangiliwa na maelfu ya wakazi waliokuwa eneo hilo, Rais Magufuli alikumbushia msimamo wake kuhusu Shinyanga akieleza kuwa hadi leo (juzi) kuna wafanyakazi hewa 226, mahali ambako walisema wafanyakazi ni sifuri, hivyo kuwaomba viongozi ambao wanataka kufanya kazi na Serikali yake wajipange kuyaondoa mabaya yaliyo kwenye maeneo yao akisema wananchi wameteseka mno.

Makonda hajaridhika watumishi hewa 71 Dar

Jana, akizungumzia suala hilo la watumishi hewa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwaagiza wakuu wa wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala kusimamisha shughuli zao kwa muda ili kulivalia njuga suala la watumishi hewa kwani bado hajaridhika na watu 71 waliopatikana hadi sasa.

Akizungumza wakati akizindua kampeni ya upasuaji watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), Makonda alisema tayari watumishi hewa 34 katika Wilaya ya Kinondoni wameshafunguliwa jalada.

“Nalipongeza jeshi la polisi kwa kumkamata mtu mmoja ambaye alikuwa anajipatia mshahara kwa njia ya udanganyifu, mpaka sasa yupo mikononi mwa vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua anazostahili kuchukuliwa,” alisema.

Makonda alisema Dar es Salaam ni miongoni mwa mikoa yenye watumishi wengi wajanja hivyo idadi ya walio hewa aliyonayo kwa sasa hawezi kuitangaza mpaka itakapokamilika, huku akitoa maagizo makuu matatu.

“Wengi wanaonekana wapo kazini, kumbe wanafanya shughuli nyingine, mwisho wa siku wanajiingizia kipato, nikaomba kuongezewa muda mbele ya Waziri (George) Simbachawene (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi), kadri tunavyoendelea idadi inazidi kuongezeka, tumeona ni vyema kuujulisha umma hatua ambazo tumeanza kuzifanya,” alisema.

Alisema ameiomba Utumishi kumpatia utaalamu zaidi ili wajanja wanaopenya wapate nafasi ya kuwabaini mapema.   

Chris Brown Akiri Alitaka Kujiua Kwa Sababu ya Penzi la Rihanna

Chris Brown amesema alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.

Katika kipande kifupi cha makala yake ya ‘Karibu katika maisha yangu’,mwanamuziki huyo wa mtindo wa R & B amesema uhusiano wao ulikuwa kama ndoto lakini akajihisi kama hayawani.

“Nilikuwa katika kilele cha dunia,nyimbo zangu zikiongoza,nikapendwa na wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui wa umma,” alisema Chris Brown.

Kesi yake ilisitishwa mwaka jana baada ya jaji mmoja kusema kuwa nyota huyo amekamilisha mahitaji yake yote na kufunga kesi hiyo rasmi.

Pia kwenye makala hiyo inayowaonyesha Jennifer Lopez,Usher,Mike Tyson,Jamie Fox na Rita Ora, Chris Brown anasema, “Nilihisi kama nyota, lakini nilijiharibia. Nilikuwa nikilala.Sikuweza kula,nilijihisi maarufu,” alikiri.

Source: BBC

Dereva Afa Maji Akijaribu Kuvuka Mto Kwa Kutumia Gari, Morogoro

Dereva tax aliyejulikana kwa majina ya Shakiru Hashimu mkazi wa Mdaula Ngerengere mkoani Morogoro amekufa maji baada ya kusombwa akiwa ndani ya gari wakati akijaribu kuvuka mto Ngerengere.

Dereva huyo alikuwa akivuka mto huo ukiwa umefurika maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.

East Africa Radio imefika katika eneo la tukio na kukuta kikosi cha jeshi kikifanya uokozi wa kuopoa mwili na gari lililo zama katika mto ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiomba serikali kuweka kingo za vyuma pembeni mwa daraja hilo ili kuzuia ajali za kutumbukia magari…

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tukio hilo ni la kusikitisha ambapo amewatahadharisha wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini wakati wanapovuka mito kutokana na mito mingi kujaa maji.

Rais Magufuli Atoa Somo Kwa Waandishi wa Habari..Awaomba Waitangaze Tanzania..Majirani Waache Kutangaza Maliasili za Tanzania Kuwa ni zao

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo juzi wakati wa uzinduzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni ambalo litakua mfano Afrika mashariki, huku akiwaomba Kuandika kwa kuitangaza nchi Kwanza

Dkt. Magufuli amesema kuwa kama waandishi wasipoitangaza Tanzania hakuna mwingine wa kuweza kufanya hivyo na ndio maana hata nchi jirani wanadiriki kunadi maliasili za Tanzania kuwa zinapatikana nchini kwao.

Aidha rais Magufuli amewaomba wahariri wa habari kuweka kurasa za mbele habari za maendeleo pia sio kila baya ndio ziwe katika ukurasa wa mbele bila kujali mazuri yaliyofanyika kwa wakati huo.

“Kwa ndugu zangu waandishi ninawaomba muitangaze Tanzania, muitangaze Tanzania mmuipende Tanzania, tusiwe wepesi wa kuandika mabaya tu ya Tanzania kila baya lipo kwenye front page zuri hakuna”Rais Magufuli alisema

Khari sio shwali, Lugumi...Majibu ya Jeshi la Polisi Hayarizishi..Sasa Ripoti Kutinga Bungeni


Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) haijaridhishwa na majibu yaliyotolewa na maofisa wa juu wa Jeshi la Polisi kuhusu Mkataba wa Lugumi Enterprises, na hivyo kamati hiyo imeamua kuunda kamati ndogo leo itakayochunguza kwa undani sakata hilo  ambapo ripoti  ya  uchunguzi huo itawasilishwa bungeni kama ilivyokuwa sakata la Escrow.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata  kutoka chanzo cha kuaminika, PAC haikuridhishwa na majibu ya hoja nyingi zilizotolewa na watendaji wakuu akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu mkataba wa Lugumi baada ya kukutana nao jana mjini Dodoma.

“PAC imelazimika kuunda kamati ndogo kesho (leo), itakayokuwa na nguvu kuhoji mambo yote ukiwemo mkataba huo kwa sababu majibu yaliyotolewa hayakuridhisha,” kilieleza chanzo hicho.

Kiliongeza kuwa baadhi ya mambo yanayokanganya PAC ni kufahamu nani mkweli kati ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kupitia taarifa ya ukaguzi na maelezo ya Jeshi la Polisi kuhusu gharama za mkataba.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, taarifa ya CAG inaonesha kuwa mkataba huo ni wa Sh bilioni 37.742 wakati maelezo yaliyotolewa na viongozi wa Jeshi hilo walipohojiwa na PAC hiyo jana, walisema ni Sh bilioni 37.163.

Hivyo kuwepo kwa tofauti ya zaidi ya Sh milioni 578.972. Aidha, utata mwingine ni jeshi hilo kukosa maelezo ya kwa nini katika kutafuta mzabuni kwenye mradi huo, walitumia mfumo wa mzabuni mmoja badala ya wengi.

Chanzo chetu kilisema katika mahojiano na viongozi hao wa polisi, walishindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza kwa nini kitengo cha manunuzi cha jeshi hilo walitumia mfumo huo.

Hivyo kutokana na utata huo, Kamati hiyo imeamua kukutana na Spika leo ili kumtaarifu hatua waliyofikia ya kuunda Kamati Ndogo.

Juzi, taarifa ya Utekelezaji wa Mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises ulioshinda zabuni mwaka 2011 ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi vya wilaya nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37, ulitua ndani ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na kuanza kujadiliwa.

Akizungumza  juzi bungeni, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema taarifa ya utekelezaji wa mkataba huo ilifikishwa bungeni Jumatatu na juzi asubuhi wamepewa na wakaanza kuujadili.

Awali, Aprili 5, mwaka huu mjini Dar es Salaam, Kamati hiyo ilitoa siku saba kuanzia siku hiyo kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi iliyopewa zabuni ya kufunga mashine 108 katika vituo tajwa nchini ila hadi sasa ni vituo 14 tu ndivyo vilivyofungwa mashine hizo.

Hatua hiyo ilikuja baada ya kamati hiyo kukutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu za jeshi hilo za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kubainika kuwa na ukiukwaji wa utekelezaji wa mkataba huo.

Ukiukwaji wa utekelezaji wa mkataba huo mwingine ni pamoja na kampuni hiyo kulipwa asilimia 99 ya fedha zote za mkataba huo wenye thamani ya Sh bilioni 37, huku kazi iliyofanywa ni chini ya robo.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 21,


Sasa hii kiboko, Mrema..Aamua Kumfuata Magufuli Dar es Salaam ili Ampe Kazi..Adai Kuna Majipu Anayajua Akayasafishe

Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha TLP na aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Vunjo, Agustino Mrema anatarajia kusafiri kuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kumpongeza Rais Magufuli na kumkumbusha ahadi aliyompa mwaka jana ya kumpatia kazi Serikalini.

Akizungumza kupitia kipindi cha Sun Rise kinachoruka kupitia Times fm, Mrema amempongeza Rais kwa jitihada za ukusanyaji kodi na kupambana na Ufisadi kwa nguvu.

“Tuweke itikadi pembeni Rais wa sasa anaweka juhudi katika kukusanya kodi, na mimi nilikuwa napiga nalo sana kelele hili swala, ila akipewa ushirikiano baada ya miaka mitano tutasheherekea mafanikio yake.

“Wiki ijayo natarajia kuja Dar, na nafikiri nitaonana na Rais kwanza nimpongeze alafu nimsisitize anipe nafasi kuna sehemu nazijua tuzisafishe, siwezi kusema mpaka nionane nae ndio nitamueleza”.

Mrema pia alijivunia rekodi yake ya uongozi katika Serikali ya Tanzania, kama kigezo kimoja wapo cha kumpatia ‘Chambirecho’ ya kupewa nafasi katika Serikali ya Magufuli.

HATIMAYE Barakah Da Prince Amvisha Naj ‘Pete ya Uchumba'

Barakah Da Prince ambaye kwa sasa amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa kike, Naj, amedai kupiga hatua zaidi kuelekea kwenye uchumba.

Wamefunguka exclusively kwa Bongo5 kuhusu uhusiano wao:

“Yeah ni kweli mimi na Naj tuna uhusino na hadi kwetu nimeshamtambulisha na yeye kwao najulikana na pia nimemvisha pia pete, sio ya uchumba ila ni Promise Ring,” amesema Barakah.

“Ndio hivyo yaani kuna kazi pia ambazo tumefanya ila hazitatoka sasa hivi hadi kwanza kila mtu atoe single yake halafu ndio itakuja hiyo ngoma ya pamoja mimi na Naj,” ameongeza.

Kwa upande wake Naj amesema:

Ni kweli Barakah amenivisha pete kama alivyosema. Kwangu ni furaha sana maana nimeshakuwa na mahusiano yaliyopita lakini sikuwahi kufanya kitu kama hiki. Naona kabisa kuwa mahusino haya ni ya ukweli na naona kuna malengo kabisa, nafurahia kwakweli.”

“Bado hatujaanza kuishi wote ila muda mwingi tupo pamoja, nafurahia mahusiano yangu ya sasa. Ni kweli tumefanya ngoma ya pamoja lakini haitatoka sasa hivi mimi natakiwa niachie ngoma yangu na pia nishoot video, halafu pia nitarudi Uingereza mara moja, kuna vitu vyangu kule then nitarudi tena Bongo.”

Diamond Platnumz Anunua Nyumba Mpya Dar es Salaam Maeneo ya Sala Sala...Bei Aliyonunulia Ipo Hapa


Diamond platnumz ameendelea kuonyesha yeye ni msanii wa kuigwa baada ya leo hii kununua nyumba mpya iliyopo dar es salaam maeneo ya salasala mwanzo
Nyumba hiyo imemgharimu diamond zaidi milion 100 za kitanzania.
Wasanii wengine wanapwa kuekeza kwenye ardhi ili kesho yake wasikose pakujificha.
Hongera sana kijana diamond una umri mdogo lakini unajitambua 

TAZAMA VIDEO Jinsi Wenje Alivyolipuaga Ufisadi wa Wilson Kabwe Mwanza...Lakini Hakuna Hatua iliyochukuliwa...Leo Kailiza Dar Pia

Mkurugenzi  wa Jiji la Dar es Salaam aliyesimamishwa kazi Jana, Wilson Kabwe kumbe alishawahi kutuhumiwa na Ufisadi mwingine alioufanya Jijini Mwanza, Tuhuma hizo zilitolewa na Wenje aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana kipindi cha awamu ya nne...

Tazama Video hii Jinsi Wenje alivyolipua Ufisadi wa Wilson Kabwe Mwanza:

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 20,



Tazama takwimu ya redio na runinga zinazocheza nyimbo nyingi Tanzania

Kampuni ya kusimania haki miliki za wasanii, Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) Jumanne hii imetoa takwimu ambazo zinaonyesha ni redio gani na runinga nchini ambazo zinaongoza kucheza nyimbo nyingi kuliko matangazo.
12974403_802515133225257_6646937415794539027_n
12974403_802515133225257_6646937415794539027_n
CMEA kupitia facebook, walipost hiyo hapo juu na kuandika:
12998623_805018622974908_2015643507876834573_n
Tambua vituo ishirini bora vya runinga na redio vilivyoongoza kucheza Muziki kwa wingi mwezi Machi, Choice FM yashikilia nafasi ya kwanza ikifuatiwa na TBC International.
12998623_805018622974908_2015643507876834573_n
Uwiano wa idadi kati ya nyimbo zilizochezwa na matangazo yaliyorushwa katika luninga zetu hapa nchini kwa mwezi Februari. EATV imeongoza kwa kucheza nyimbo nyingi kuliko matangazo ikifuatiwa na Clouds TV, Zilizobaki zinaongoza kwa upigaji wa matangazo.
13012799_805019946308109_3457103951552612697_n
13012799_805019946308109_3457103951552612697_n
Uwiano wa uchezaji nyimbo na matangazo katika stesheni za redio jijini Dar es Salaam kwa mwezi Februari huku Clouds FM na RFA zikiongoza kwa kurusha matangazo. Stesheni zilizobaki zinapiga muziki kwa asilimia kubwa kuliko matangazo.